Baada ya Uganda kuwekewa vikwazo vya kiuchumi na Marekani kwa kukataa ushoga, kuna taarifa za chini chini kwamba Marekani ina mpango wa kuzitaka nchi za Kenya na Tanzania kutunga sheria zinazounga mkono mambo ya ushoga, kama ilivyozilazimisha nchi hizo kutunga sheria zinazopinga vitendo vya ugaidi.
Msemaji wa wa serikali ya Marekani ameilaani Uganda kwa kutunga sheria inayokataza vitendo vya kishoga na pia kuwanyanyasa wapenzi wa jinsia moja. Ikulu ya White house imelaani sheria hiyo ikisema kuwa inakwenda kinyume na uhusiano kati ya nchi hizo ikitoa wito wa sheria hiyo kufutiliwa mbali. Waziri wa mambo ya nje John Kerry, amefananisha sheria hiyo na sheria za utawala wa zamani wa kinazi nchini Ujerumani.
Ndugu zangu, hivi kweli ikiwa Marekani itavalia njuga suala hili kuna uwezekano Tanzania kugoma kufanya hivyo? Nina wasiwasi kama kweli Tanzania itakubali kukosa fedha za maendeleo kwa sababu tu ya kugoma kuunga mkono vitendo vya kishoga, hasa ukizingatia uhaba wa kifedha unaoikabili nchi. Ngoja tusubiri tuone lakini sina uhakika kama Tanzania ina ubavu wa kukataa ushenzi huo kwa kuwa nakumbuka ilikuwa nchi ya kwanza kutunga mswada wa ugaidi kabla ya nchi nyingine za afrika mashariki kukubali kufanya hivyo.
Nina imani kwamba serikali ya Kenya inawezea kukataa ushoga kama ilivyofanya Uganda lakini ni vigumu sana kwa Tanzania kukataa kwa kuhofia kuharibu uhusiano na wafadhili wake na kukosa fedha za misaada ya maendeleo ya wananchi. Mungu epushia mbali ushenzy huo usifike Tanzania.
0 Comments