Binadamu wote wenye mafanikio duniani hawachoki kutafuta!
Na: Meshack Maganga- Iringa.
Ndugu zangu, awali ya yote ninapenda kutuo shukrani zangu za dhati kwa wasomaji walioniandikia na kunipigia simu na jumbe fupi nyingi sana, nilipoandika makala ya tarehe 8.4.2014 niliyoipa kichwa cha 'Unaweza kujiajiri kupitia kilimo cha vitunguu' Nilipokuwa ninandika makala ile ofisini kwangu, Iringa niliona nikama niandika mambo ya kawaida tu, maana mimi ni mzoefu, kumbe yalikuwa mambo mhimu sana na yaliyo wasaidia watanzania wengi, nilisafiri kwenda Kyela nilipokuwa ndani ya gari nilipokea jumbe fupi 442 na barua pepe nyingi sana zaidi 56, nilipigiwa simu nyingi, nilijitahidi kujibu baraua pepe zote kuna
baadhi ya jumbe fupi zilinigusa sana, Msomaji mmoja alinitumia ujumbe huu "Ni furaha gani niliyojawa baada ya kusoma maelezo yako ya kilimo, mi ninasema umeletwa na Mungu ili mimi nifanikiwe…" Nimejifunza sana na nimepata marafiki wengi sana kupitia ile na baadhi yao wamechukua hatua za kuanza kulima kilimo cha vitunguu na baadhi yao wameanza kuwekeza kwenye kilimo cha miti, baadhi walikuja Iringa wakatembelea mashamba ya miti wakajifunza wakachukua hatua.
Kwa kifupi sana leo nitaongelea umhimu wa kuzichangamkia na kuendelea kuzitafuta fursa za mafanikio zilipo ndani ya nchi yetu yenye amani na kila aina ya fursa, hii ni kwa sababu wengi wetu ama kwakufanya uzembe na kujipa moyo kwamba muda bado upo, tumekuwa tukipoteza fursa hizo. Ama wengi wetu tumezikosa fursa hizo kwa visingizio lukuki, ama wengi wetu hatuna taarifa sahihi ya kile tunachokitaka, na wengi wetu tumekuwa na mipango mingi sana na wengine tumepoteza fursa kwakuwa 'bize' na ndoto za wenzetu na kushabikia kila kinachotoea mtaani kwetu.
Dunia hii na nchi yetu kwa ujumla wake imepiga hatua kubwa za kimaendeleo nahivyo kuwezesha fursa za kila aina kuwa wazi, kwa sasa kilimo kimeajiri watu wa kada zote waliosoma na wasiosoma, ongezeko la watu mjini na vijijini imesabaisha uhitaji mkubwa sana wa chakula, kila utakacho amua kukifanya kwenye sekta ya kilimo kitakuletea pesa, utajiajiri na kupata pesa ya kutosha. Lakini unapoisikia fursa ya kilimo nenda ukaifanye ama ujifunze uamue kuifanya ama kutoifanya uamue kufanikiwa ama kushindwa ama uendelee kupiga kelele na kutoa lawama kila siku.
Dunia ya sasa ni dunia ya wanadamu wanaojua ni kitu gani wanaweza.Siyo dunia ya kufuata mkumbo wala upepo na matukio ya kijamii Wapo wanaopenda kuwa madaktari, wapo wanaopenda kuwa waimbaji nk. Kila mtu ana kitu anachopenda kinachomfanya acheke akiwa duniani. Tafuta kitu unachokipenda na kiendeleze, kitakuletea mafanikio, usisubiri umalize masomo yako, ama ukifikisha umri wa kuacha kazi ndio uaanze kutafuta nini cha kufanya utajuta hapo baadae.
Ukitaka kuishi kimafanikio kiroho,kimwili na kijamii kuwa na njaa ya fursa na mfanikio kila kila siku. Binadamu wote wenye mafanikio duniani hawachoki kutafuta maarifa kwa kusoma vitabu, kuuliza na kujifunaza, na hata kuhudhuria mafunzo ya kuwaendeleza mara kwa mara. Mwaka huu mwezi wa tatu, nilikutana na mjasirimali Paul Masatu akanipatia elimu ya jinsi ya kubadili mtazamo wako nilikaa nae nilimwuliza maswali mengi sana, elimu ile ya kujitambua imenisaidia sana kubadilisha mtazamo wangu na nimefanikiwa kujenga mtazamo wangu kwa kiasi kikubwa nabado ninajifunza kwa kusoma vitabu vya waliofanikiwa.
Mjasiriamali na mwalimu wa mbinu za mafanikio, Paul Mashauri amenipa funzo kubwa sana kwenye maisha yangu ninamshukuru sana anasema, "Ukitaka ufike juu katika maisha lazima ujifunze maisha ya walio juu, wanafanya nini, wanawaza nini, wanakaa wapi, wanakula wapi, wanaongea na akina nani, wanaongeaje, wanakutana wapi, kwa nini, wanapanga nini, wanapanga na nani nk. Huwezi kutaka kuonana na CEOs wakati mchana kutwa unashinda manzese uwanja wa fisi na usiku unakesha Kamanyora baa".
Niliwahi kuandika kwenye ukurasa wangu wa facebook kwamba, Siri kubwa ya watu wenye mafanikio duniani, ni kuwa hawaogopi maisha, wapo tayari kuumia kwa kuchagua maisha wayatakayo. Chagua kipengele mojawapo cha kijasiriamali unachotaka kukifanya na ukifanye kweli kwa moyo wote. Jiendeleze kila siku katika ulilochagua kiasi ambacho utavunja mipaka na kuweka rekodi yako. Chagua kufanikiwa ama kushindwa.
Na ndivyo ilivyo unapotafuta fursa, huwezi kutafuta fursa kwa kusoma mambo yasiyoendana na fursa unayoitaka, kwa mfano kama wewe ni binti uliyehitimu chuo na ndoto yako ni kwa mjasiriamali kwenye kipengele cha saluni, nenda ukawatafute wenye saluni kaa nao ujifunze kwao, unataka kulima vitunguu watafute walima vitunguu wakupatie mbinu. Huwezi kuwa na ndoto ya kuanzisha mgahawa halafu ukataka ushauri kwa mfugaji huenda akakukatisha tamaa na ndoto yako ikapotea kabisa. Kama ndoto yako ni kuanza ufugaji wa kuku watembelee wafugaji wa kuku, kaa nao waulize maswali walianzaje ili upate taarifa sahihi za ufugaji.
Ninakumbuka Mwalimu wangu wa somo la kemia wakati ule nikiwa kidato cha kwanza, alitufundisha kwamba, chuma usipokitumia kwa muda mrefu hupata kutu. Ndivyo ilivyo kwa binadamu usipoitumia akili yako vizuri, akili yako itapata kutu ya aina fulani, utakuwa mtu wa lawama kila leo, utawasingizia ndugu zako, rafiki zako, utawasingizia viongozi wako nk. Binadamu wanaotumia akili yao vizuri hawachoki kutafuta wanachokitaka kwenye maisha yao. Kuna baadhi yetu ambao ama kwakufanya uzembe hawatumii akili yao kutafuta mambo mazuri, wanaona ubaya kwa kila fursa inayopita mbele yao.
Nimesoma Kitabu cha Mwalimu Mwakasege amesema kwamba, "watu wengi wamekuwa wakifikiri ya kuwa Mungu ndiye aliyewapangia kuwa maskini. Na hata wakristo wengine kudiriki hata kuuona umaskini kama sehemu ya utakatifu na unyenyekevu". Ina maana mpaka sasa kuna watu wanaofikiri kwamba umaskini ni kama sifa Fulani hii ni hatari.
Achana na mawazo yatakayo kukatisha tamaa, achana na marafiki wanaokupotezea muda wako, walalamishi, jenga urafiki na waliofanikiwa. Ni mpango wa Mungu ni kukuona wewe ukishi maisha ya furaha, maisha ya utele na mafanikio katika Nyanja zote za kiuchumi na kijamii na kiroho. Kama kuna kitu kinaitwa bahati, basi asilimia 90 inakwenda kwa wale watafutaji na wachapakazi na wasiokata tamaa. Ninawatakia mafanikio mema.
BINADAMU WENYE MAFANIKIO HAWACHOKI KUTAFUTA
0713486636 email meshackmaganga@gmail.com https://www.facebook.com/Fresh-Farms-Trading
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.
0 Comments