TAARIFA KWA UMMA
Wizara ya Kazi na Ajira inapenda kuutaarifu Umma kwamba Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete amemteua Bw. Juma Ally Muhimbi kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii (SSRA) kuanzia tarehe 28 Aprili 2014 kwa kipindi cha miaka mitatu. Uteuzi huu umefanyika kwa mujibu wa Sheria ya
Usimamizi na Udhibiti wa Hifadhi ya Jamii Na. 8 ya mwaka 2008.
Aidha kwa mujibu wa Sheria hiyo, Waziri wa Kazi na Ajira Bibi Gaudentia M. Kabaka (MB.) Amewateua wafuatao kuwa Wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi:-
Prof. Hamsa F. Kiko - (Mwakilishi wa TUCTA)
Bw. Mchafu A. Chakoma - (Mwakilishi wa TUCTA)
Bibi Jayne K. Nyimbo - (Mwakilishi wa ATE)
Bw. Jones M. Sikira - (Mwakilishi wa ATE)
Bw. Sylvester A. Mwakitalu (Mwakilishi wa Mwanasheria Mkuu wa Serikali)
Bw. Saul H. Kinemela - Kamishna wa Kazi - Wizara ya Kazi na Ajira
Bw. Mihalale E. Mwakimbina - Kaimu Msajili wa Hazina - Wizara ya Fedha
Bw. Charles M. Chenza - Mwakliishi wa Sekta Binafsi
IMETOLEWA
NA
RISHIWAN WEMA
MSEMAJI
WIZARA YA KAZI NA AJIRA
13/05/2014
-- Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.
0 Comments