[wanabidii] ACT - TANZANIA Kukabidhiwa Cheti cha Usajili wa Kudumu na Msajili wa Vyama vya Siasa Mei 5, 2014

Saturday, May 03, 2014
ACT - TANZANIA! TAIFA KWANZA!

Napenda kuchukua fursa hii kuwataarifu wana ACT-TANZANIA nchi nzima kwamba chama chenu kitakabidhiwa Cheti cha Usajili wa Kudumu na Msajili wa Vyama vya Siasa Mei 5, 2014 kama ilivyopangwa. Na kwa hiyo natangaza kwamba Birth Day ya ACT - TANZANIA ama ACT DAY itakuwa ni Mei 5 ya kila mwaka. 

Naomba tuwe na subira mpaka hapo kamati ya muda ya kitaifa itakapoketi sikuchache zijazo kwa ajili ya kupanga ratiba na program ya chama kuanzia sasa mpaka Dec. 2014 ikijumuisha uchaguzi mkuu wa kwanza wa chama, uzundizuzi rasmi wa chama na maandalizi ya ushiriki wetu kwenye chaguzi za kiserikali zilizo mbele yetu ikiwa ni pamoja na uchaguzi wowote mdogo utakaotokea hivi karibuni. 

Kazi kubwa tuliyonayo kwa sasa ni kukieneza chama mpaka ngazi za chini kabisa. Tunafanya kila juhudi kuchapisha kadi mpya na bendera mpya kwa ajili ya kazi hiyo. Wakati zinasubiriwa hizo, endeleeni kutumia hizo zilizopo na pengine kutumia madaftari kuorodhesha wanachama wenu kadi zitakapokuja mtawapa. Mkoa wowote ambao tayari una wanachama wa kutosha lakini hawajawa na viongozi wa muda (waratibu) wawasiliane na Naibu Katibu Mkuu Bara (Leopold Mahona - 0758409670 / 0787457970) ama Katibu Mwenezi Taifa (Masaga Mohamed Masaga - 0718388888 / 0766845424) kwa ajili ya maelekezo ya namna ya kuchagua waratibu wa muda. Rasimu ya mwisho ya Katiba inakamilishwa, ikishakuwa tayari itawasilishwa kwenye kamati ya taifa na baadaye kwa wadau wote ili mpate kutoa maoni yenu kabla ya kuja kupitishwa rasmi kwenye mkutano mkuu maalum. 

Nawatakia heri na Baraka za Mwenyezi Mungu Subh-a-annah wat-a-allah katika ujenzi wa chama mbadala kwa ajili ya TANZANIA TUITAKAYO!!!

MABADILIKO NA UWAZI! CHUKUA HATUA!

Maingu Samson Mwigamba,
Katibu Mkuu.

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

Share this :

Related Posts

0 Comments