[wanabidii] Salamu za Pasaka 2014 kutoka CCM-Uingereza

Sunday, April 20, 2014
CHAMA CHA MAPINDUZI - TAWI LA UINGEREZA – UNITED KINGDOM

Website ccmuk.org, Blog ccmuk.org/blog, Facebook page Chama Cha Mapinduzi uingereza, twitter CCMUK1

Contacts Phone +44 74 04 863333, +44 7545 213515
E-mail – itikadi-uenezi@ccmuk.org

Chama Cha Mapinduzi- London – Uingereza kinaridhia Salaam za CCM Makao Makuu kuungana na Wakristo- Watanzania na Ulimwenguni kote kuwatakia kila la kheri na fanaka katika kusherehekea Sikuu Kuu ya PASAKA 2014.

Aidha CCM UK inayo imani kubwa kuwa Sherehe hii ya Pasaka itakuwa kigezo cha kuwakaribisha Watanzania wa Imani zote kujitazama kwa wongufu na kuridhia misingi mikuu ya Uhuru, Muungano wetu na Umoja wa Taifa letu.

CCM UK inaungana na Watanzania wote kukememea dhidi ya vichocheo vya aina zote vinavyohatarisha umoja wa TAIFA LETU, usalama wa raia na mali zao, uhuru wao wa kuabudu na kusujudu ndani na nje ya mipaka ya Tanzania.

Kwa kuwa Dhamira kuu ya Pasaka ni kujenga Upendo, Mshikamano, Umoja na Uhuru, hasa katika kipindi hiki cha kutafakari mchakato wa Kupata KATIBA MPYA yenye kukidhi kiu ya maendeleo kwa Wananchi Kiuchumi na kimaendeleo kama Taifa moja, CCM UK inawatakia kila la kheri katika kusheherekea sikukuu hii muhimu kwa Wakristo wote Duniani kwa Amani na Utulivu.

MUNGU IBARIKI TANZANIA.

Imetolewa na Abraham Sangiwa - Idara ya Siasa na Uenezi.

CCM – TAWI LA UINGEREZA - UNITED KINGDOM.

20th April -2014

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

Share this :

Previous
Next Post »
0 Comments