[wanabidii] SABABU ZA UKAWA KUSUSIA BUNGE LA KATIBA

Wednesday, April 16, 2014

Wajumbe wa bunge la kutoka vyama vya upinzani vya CUF. Chadema, NCCR , Dp, NRA, NLD na Udp ambao wanaunda umoja wao unaojulikana Kama Ukawa wamesusia bunge na kuondoka bungeni kwa kushindwa kuvumilia hoja zinazotolewa na wapinzani wao wakuu kutoka chama tawala.

Mwenyekiti wa CUF Prof. Ibrahim Lipumba ameliambia bunge la katiba takriban saa 10.30 leo jioni kuwa wamechoka kusikiliza hoja za wajumbe wanaotaka muundo wa serikali mbili kinyume na mapendekezo yaliyotolewa na rasimu ya Katiba iliyoandaliwa na Tume ya Jaji Warioba.

Mara baada ya kumaliza kuzungumza na kuwaaga wajumbe wa bunge Hilo kwa niaba ya wajumbe wa Ukawa prof. Lipumba aliwaongoza wajumbe wenzake wa Ukawa kutoka nje ya bunge.

Hata hivyo Wajumbe hao walioaga bunge kupitia prof Lipumba walitoka bungeni kuelekea katika ukumbi wa msekwa kufanya kikao cha ukawa huku Makamu Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba mh. Samia Suluhu Hassan ameendelea kuliongoza bunge Hilo kwa wajumbe kuendelea kuchangia.

Wengi wa wajumbe kutoka kundi la 201 wapo bungeni wakiwemo wale wa kundi la viongozi wa dini.

Bunge maalum la Katiba Jumatatu saa Saba mchana lilimaliza kupokea taarifa kutoka kamati 12 zilizokuwa zinajadili sura ya kwanza na Sita zinazohusu muundo wa muungano kazi iliyofanywa kwa Siku Tatu.

Wakati wa uwasilishaji wa taarifa hizo za kamati kundi la wajumbe wachache likiongozwa na wana ukawa lilipewa masala 6 kufafanua hoja zao zilizosomwa na wenyeviti wa kamati hizo kwa niaba yao fursa ambayo waliitumia kueleza Maoni yao ya kukubaliana na muundo wa serikali 3 uliopendekezwa na Tume ya Jaji Warioba.

Hoja walizotoa ni pamoja na muungano uliopo haukuhalalishwa hususan na serikali ya mapinduzi zanzibar, kutokuwepo kwa hati ya muungano, Mwalimu Nyerere alitumia ujanja ujanja kutekeleza shughuli za muungano, waliozoea vya kunyonga vya kuchinja hawaviwezi kwani wameishi kwa uongo kwa zaidi ya miaka 50 yaani nusu karne na sasa wamefikia mwisho wake na mengine mengi.

Jumatatu mchana wajumbe wa bunge la Katiba walianza kuchangia kwa hoja zilizoonyesha kuwa muungano uliodumu kwa miaka zaidi ya miaka 50 ni halali na jana Jumanne Serikali ilitoa hati ya muungano na wajumbe hao wa kundi la waliowengi kueleza hoja zilizotolewa na wana Ukawa za kuwadhalilisha waasisi hazitendi haki kwa waasisi hao.

Bunge Maalum la katiba linaloendelea hivi sasa mjini Dodoma likishindwa kupitisha rasimu ya katiba jamhuri ya muungano wa Tanzania itaendelea kutumia KATIBA ya zamani iliyorekebishwa Mara ya mwisho 1977

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

Share this :

Previous
Next Post »
0 Comments