[wanabidii] NJIA ZA KULINDA UTAMBULISHO WAKO MTANDAONI

Saturday, April 05, 2014
NJIA ZA KULINDA UTAMBULISHO WAKO MTANDAONI

UTAMBULISHO MTANDAONI NI NINI ?

Huu ni utambulisho wowote unaohusu wewe kwa njia ya mtandao jinsi unavyotumia huduma mbalimbali kwa kutumia utambulisho wako kama jina , namba za siri , barua pepe au Namba za simu .

Kadri ya siku zinavyozidi kusonga dunia inazidi kuwa kijiji , tunapata vifaa vya kurahisisha mawasiliano na kazi zetu mbalimbali na tunazidi kujaza taarifa kwenye mitando mbalimbali haswa ya kijamii kwa kutumia utembulisho wetu wa uwongo au ukweli .

Wahalifu wengi wameweza kutumia udhaifu wa baadhi ya watu katika utumiaji sahihi wa huduma za mawasiliano na kuweza kuwaibia taarifa muhimu au hata kufanya uharibifu Fulani .

Udhaifu huu unaweza kuzuiwa au kupungua kutokana na elimu kama hizi tunazoshiriki kutoa kwa watu .

UNALINDAJE UTAMBULISHO WAKO MTANDAONI ?

Kwanza ni kuhakikisha kifaa au vifaa unavyotumia kuingilia kwenye mtandao havina shid yoyote na zaidi vimeboreshwa kwa kufanyiwa updates kama ni antivirus au operating system .

Usiingize program usiyoijua au kujua maelezo yake kwenye simu au kompyuta pia usitumie leseni za program zilizochakachuliwa labda kama unajua unachofanya .

1 – Uwe makini na taarifa unazoingiza au kushare na watu mtandaoni haswa mitandao ya kijamii , mhalifu anaweza kutumia taarifa hizo kukuibia au kuibia wengine au kuleta maafa kwa njia mbalimbali kama sio leo hata kesho .

Vitu kama tarehe ya kuzaliwa , vitu unavyopenda , mke/mume wako , jina la paka au mnyama unayempenda , watoto ni hatari wakati mwingine .

2- Weka password au neno la siri kwenye vifaa vyako kama ni simu au kompyuta na unaweza kuweka password kwenye folders au file na progam muhimu ndani ya kompyuta au simu yako , neno la siri liwe na mchanganyiko wa herufi kubwa , ndogo na namba isifanane na vitu unavyopenda au mahala ulipo .

3 – Kama unanunua vitu kwa njia ya mtandao hakikisha unazijua tovuti hizo na njia rahisi zaidi ni Antivirus unayoitumia kama uko updated ni rahisi kuwa na database ya tovuti zote bandia kwahiyo ukiingia itakublock au itakuuliza maswali .

4 – Weka alert kama ni kwenye simu au kompyuta au huduma nyingine kwa njia ya mtandao kama chochote kikibadilika basi uweze kuthibitisha kwa njia ya simu au email kwa kuingia , siku hizi benki nyingi zinahuduma hizi za sms na emails nyingi zimeunganishwa na namba za simu kwahiyo zinafanya kazi pamoja .

5 – Kama hujaelewa taarifa yoyote kama muamala wa fedha bora uulize mapema kwa watoa huduma wako wa fedha na haswa kama muamala huo hujauruhusu wewe .

6 – Badilisha Password zako mara kwa mara na usipende kushare na watu .

7 – Usiazimishe vifaa vyako vya mawasiliano kama simu na kompyuta kwa watu usiowajua au kuwaamini , pia usipeleke vifaa hivyo kwa mafundi usiowaamini na kama ukiacha basi hakikisha taarifa muhimu hazipo na bora aje kutengenezea kwako kama ni mbovu .

8 – Kama kifaa chako cha kuhifadhia taarifa kimekufa au kuleta hitilafu usitupe hovyo , ni kuharibu mazingira na pia kinaweza kuokotwa na kutolewa hizo taarifa .

9 – Kama una kampuni ni bora kusajili huduma za email kwa kutumia rajisi ya Tanzania ya dot co dot tz kwa ajili ya mawasiliano yako yote ya njia ya mtandao utajiepusha na mengi .

10 – Usipende kusambaza ujumbe wa bure haswa kwa njia ya barua pepe , hiyo ni kati ya njia rahisi ya kuvunwa barua pepe yako na mawasiliano yako mengine .
Hakuna vitu vya bure , kila unachokiona kwenye mtandao kina gharama zake kama sio leo ni kesho au keshokutwa au kwa watu wengine .

Ahsante 

YONA FARES MARO
0786 806028 
SONGO SONGO 


--

Yona Fares Maro

Institut d'études de sécurité - SA


--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

Share this :

Related Posts

0 Comments