[wanabidii] Mwaliko kwenye Kongamano la Muungano Chuo Kikuu cha Dar es Salaam

Wednesday, April 23, 2014
Text Box:
UNIVERSITY OF DAR ES SALAAM
Academic Staff Assembly
 
 
 
 

MWALIKO KWENYE KONGAMANO LA MUUNGANO  26 APRILI  2014                                                                                                         
Kwa niaba ya uongozi wa Jumuiya ya Wanataaluma wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kwa kushirikiana na Idara ya Sayansi ya Siasa na Utawala napenda kuwakaribisha kwenye  Kongamano la Muungano litakalofanyika ndani ya ukumbi wa Nkrumah siku ya Jumamosi tarehe 26 Aprili 2014. Kongamano hilo litaanza saa 7.30 mchana hadi saa 12 jioni ndani ya UKUMBI  WA NKRUMAH WA CHUO KIKUU CHA DARE ES SALAAM. Mada kuu ya Kongamano hilo ni, «Tujadili na Tutafakari Mustakabali wa Muungano wetu»
                                     
Kutakuwa na mada tatu za kujadiliwa na watoa mada kwenye mabano:
 
1) Chanzo au Mchakato wa Kisiasa wa kuwa na Muungano (Prof. Mohammed Bakari)
2)     Tathmini ya Miaka 50 ya Muungano (Dkt Alexander Makulilo)
3)      Mustakabali wa Muungano (Prof. Gaudence Mpangala)
 
Tunaomba kwa yeyote mwenye maoni basi asisite kututumia kwa barua pepe kwa anwani : kongamanoudasa@gmail.com.
 
 
Asanteni sana
 
Bw. Faraja Kristomus
(Katibu - UDASA)
Department of Foreign Languages and Linguistics
University of Dar es Salaam
P.O.Box 35040, Dar es Salaam
Tanzania
Mobile: +255 787 52 53 96 / +255 717 086 135

"All human beings are equal except our beliefs, tribes and thinking, which are always accidents and never the essences of our humanity. We acquire them after getting out of the wombs of our mothers".

Share this :

Previous
Next Post »
0 Comments