[wanabidii] Wauzaji wa vitabu (Maajenti) wanahitajika

Tuesday, March 04, 2014


Wauzaji wa kitabu, maajenti wanahitajika toka mikoa yote Tanzania.Sasa Kitabu cha Mbinu za biashara na maarifa ya kupata pesa na utajiri,hard Copy kiko Sokoni. Bei yake ya reja reja ni sh. 6,000 tu wakati bei ya jumla ni sh.4000 kila ajenti atapata faida ya sh. 2000 kwa kila kitabu atakacho nunua na kuuza. Vitabu vitanunuliwa na maajenti kwa pesa taslimu hakuna mkopo. Kwa wale wanaokihitaji wanaweza kufika ofisi za CPM Business Consultants, Sinza kwa Remi au wapige simu namba 0755394701. Kwa wale walioko mikoani wasihofu tunao mfumo wa kukufikia wasiliana nasi kwa kutuma pesa kwa M PESA sh. 4,000 kwa kila kitabu, simu namba 0755394701 nasi tutakutumia vitabu vyako.

Kitabu hiki kinalenga kumsaidia mtu yeyote ambaye anatafuta utajiri kwa kufanya biashara ndogondogo hadi kubwa. Pia kinatoa maarifa, mbinu na mikakati mbalimbali ya kupambana na umaskini, kinatoa elimu ya biashara na mbinu mbalimbali za namna ya kupata pesa kwa njia halali ili kukurahisishia safari yako ya kuelekea kwenye kutafuta na kupata utajiri. Kitabu hiki kina sehemu mbili, sehemu ya kwanza inaeleza kuhusu taratibu za kuanzisha biashara sheria, utafiti wa masoko, utunzaji wa hesabu za biashara na utatuzi wa matatizo ya biashara. Sehemu ya pili inaelezea kuhusu mawazo, mbinu mbalimbali za biashara unazoweza kuzifanya na kupata faida na hivyo kutajirika.

Mtunzi wa Kitabu hiki Charles P. M. Nazi ni mshauri wa masuala ya biashara na Mkurugenzi Mtendaji wa CPM Business Consultants.
Kitabu hiki ni matokeo ya utafiti na uzoefu katika kazi za ukaguzi alizozifanya kwa kuangalia matatizo ya uendeshaji wa biashara mbali mbali pamoja na ushauri alioutoa kwa watu waloomba ushauri kutoka kwake.

CHARLES NAZI
MTUNZI WA KITABU CHA MBINU ZA BIASHARA

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.

Share this :

Previous
Next Post »
0 Comments