[wanabidii] HOJA KINZANI BUNGENI: USTAARABU WA KIDEMOKRASIA NA MUAFAKA WA KITAIFA NI NYENZO YA KUPATA KATIBA BORA

Tuesday, March 04, 2014
Demokrasia ni udikteta wa walio wengi ambapo hoja inayoungwa mkono na wengi huonekana ni bora na hupewa nafasi. Hata hivyo, kuna muktadha ambao udikteta wa wengi hauna tija na badala yake ustaarabu wa demokrasia huchukua nafasi na hatimaye walio wachache hupewa nafasi na hoja yao kuwa na nguvu dhidi ya udikteta wa wengi. 

Ustaarabu wa demokrasia unahitajika zaidi mnapokua mnafanya maamuzi ambayo yanahitaji zaidi concesus (muafaka) kuliko compromise (maridhiano). Mkijenga muafaka mnaondoka mkiwa wamoja na jambo husika linakuwa la wote na mkijenga maridhiano mnamaliza mjadala wengine wakiwa wameridhia kwa shingo upande yaani mnakubaliana kutokukubaliana. 

Katiba ni ya watanzania, na mchakato wa katiba ni tukio la kihistoria kwani hili ni tukio la kwanza katika historia ya taifa letu. Tunatengeneza Tanzania ya miaka 100 ijayo. Vilevile wajumbe wa bunge wametokana na makundi tofauti bila shaka kwa lengo la kuzifanya sauti za kila kundi kusikika. 

Katika muktadha huu, ustaarabu wa kidemokrasia unahitajika zaidi kuliko udikteta wa wengi. Muafaka unahitajika zaidi kuliko maridhiano. Kukubali kukubaliana ni bora zaidi kuliko kukubali kutokukubaliana. 

Wapo wanaodhani kutoa nafasi kwa wachache kutoa hoja yao wenyewe ni kupoteza sana muda. Kwa unyeti wa mchakato huu, muda siyo hoja bali ubora wa mchakato. Wapo waliotumia zaidi ya miezi sita kuandaa kanuni za bunge maalumu katiba. Kwao ubora wa kazi na unyeti wa mchakato ulipewa nafasi. 

Wapo wanaodhani hoja ya wachache kusomwa na mkt na baadae wachache kupewa nafasi ni bora zaidi, lakini bado walio wachache wanadhani wameporwa haki yao ya kusikilizwa na kwa maana ya ustaarabu wa kidemokrasia wako sahihi. Sauti yao wanataka itoke miongoni mwao. Wanataka wapewe nafasi wapaze sauti zao pale itapobidi kwani siyo lazima kukubaliana kutokubaliana. 

Mchakato huu umejengeka katika misingi ya muafaka na unapaswa kuendelezwa katika mfumo huo. Mh. Raisi Dr. Kikwete amekua akikaa pamoja na wapinzani pale anapoona hawajaridhika ndani ya bunge kutokana na udikteta wa wengi. Kwa kuwa yeye mwenyewe ndiyo muasisi wa mchakato huo na angependa kumaliza muda wake akiwaacha watanzania katika taifa bora zaidi kidemokrasia na utawala bora duniani na kwa kuwa anajua kwamba mchakato huu ni wa kitaifa na hivyo kuhitaji zaidi muafaka kuliko maridhiano, ndiyo maana milango ya muafaka wakati wote inapaswa kuwa wazi katika kila hatua kwa mustakabali bora wa taifa letu. 

Kwa maoni yangu, ili kuepuka maridhiano na udikteta wa wengi katika muktadha huu ambao unahitaji muafaka na ustaarabu wa kidemokrasia ni vyema wachache wapewe nafasi waeleze hisia zao na baada ya hapo bunge lote litaamua kwa kupima uzito wa hoja. Jambo la msingi kanuni zitamke kwamba baada ya hoja ya wengi kuwasilishwa na wachache kupaza sauti zao, bunge litapima na kufanya maamuzi na kwamba maamuzi hayo yatakuwa ya mwisho. Hapo wataridhika na kuona kwamba wametendewa haki.

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.

Share this :

Previous
Next Post »
0 Comments