Wananchi wa Tanzania wamepongezwa kwa kufikia miaka 50 ya Muungano huku wakiulinda na kuuimarisha mpaka Leo.
Hayo yamesemwa na Balozi Job Lusinde ambaye alikuwa mjumbe wa kamati ya kutayarisha katiba ya Muungano Hivi karibuni Mjini Dodoma.
Balozi Lusinde ambaye pia alikuwa Waziri wa serikali za Mitaa katika Baraza la kwanza la Tanganyika mwaka 1961, baada ya kupata Uhuru amesema kwamba madhumuni ya kuanzisha Muungano huo ilikuwa ni kuonyesha mfano ili siku moja uwepo Umoja wa nchi za Afrika.
"Wakati tunaugana na Zanzibar kulikuwepo upepo wa kuwa na Shirikisho la Afika Mashariki, hivyo ilikuwa rahisi kuanza na Muungano wa Tanganyika na Zanzibar Kama mfano mkubwa wa kimatendo " alisema Balozi Lusinde.
Aliendelea kusema kwamba madhumuni mengine yalikuwa ni kuuimarisha uchumi wa nchi hizi mbili kwani kabla ya Muungano Zanzibar ilikuwa na watu 300,000 na Tanganyika ilikuwa na watu 8,000,000, hivyo baada ya kufunga na uchumi ukiwa unategemeana na wakaunganisha nguvu kiuchumi , jambo ambalo lilikuwa faida kwa nchi hiyo mbili.
Aidha, Balozi Lusinde alisema kwamba wakati wa kuungana walifikiria suala la usalama wa nchi hizi mbili, kwamba ni muhimu hivyo kwa kuungana kutaweza kuimarisha usalama.
Suala la mwingiliano wa kijamii pia lilichochea kuungana kwa nchi hizi mbili. "kulikuwa na mwingiliano mkubwa awa kijamii kama vile kuoleana, kutembelea a na biashara, hivyo kutokana na Wazanzibar kuishi Tanganyika na halikadhalika Watanganyika kuishi Zanzibar, suala la kuungana lilikuwa Kama liko tayari" alisema Balozi Lusinde.
Aliongeza kusema kwamba baada ya Muungano, umoja, usalama na uchumi uliimarika.
Balozi Lusinde alisisitiza suala la kuulinda na kuuimarisha Muungano wetu na kushauri changamoto zilizopo zizungumzwe na kutafutiwa ufumbuzi.
Akizungumzia uwepo wa Serikali tatu, Balozi Lusinde alisema Hanoi haja ya kuwepo maana miaka 50, ya Muungano tunaona matunda yake."serikali tatu hazina haja ya kuwepo, kwani zitaleta katika uendeshaji wake, pili serikali hizi zitakuwa na gharama ya uendeshaji wake, na tatu zitawachanganya wananchi" aliongeza Balozi Lusinde.
Balozi Lusinde alimalizia kwa kushauri kwamba Muungano wetu usiwekewe kitu chochote cha kuwavuruga Watanzania ili wasivurugike, wasitengane na wasigombane.
-- Hayo yamesemwa na Balozi Job Lusinde ambaye alikuwa mjumbe wa kamati ya kutayarisha katiba ya Muungano Hivi karibuni Mjini Dodoma.

Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.
0 Comments