[wanabidii] TAARIFA KUHUSU KUKAMILIKA KWA ZOEZI LA UTEUZI WA MAKAMU MWENYEKITI WA BUNGE MAALUM

Friday, March 14, 2014

TAARIFA KUHUSU KUKAMILIKA KWA ZOEZI LA UTEUZI WA MAKAMU MWENYEKITI WA BUNGE MAALUM


Inatolewa chini ya Kanuni ya 5(4)(a) na NYongeza ya Kanuni za Bunge Maalum za Mwaka 2014

Tarehe 12 Machi 2014 Mwenyekiti wa Muda alitangaza nafasi ya Makamu Mwenyekiti na kuelekeza wajumbe wenye sifa wachukue Fomu. Wajumbe wawili walijitokeaza na kuchukua Fomu za kugombea nafasi ya Makamu Mwenyekiti wambao ni:-

  1. Ndg. Amina Abdallah Amour; na
  2. Ndg. Samia Suluhu Hassan.
Wajumbe hao wawili wamerudisha FOmu leo siku ya Alhamisi, terehe 13 Machi, 2014 na kutimiza masharti ya uchaguzi kwa mujibu wa Kifungu cha 23(4) cha Sheria ya Mabadiliko ya Katiba, Sura ya 83 na Kanuni ya 5(2) na Nyongeza ya Kanuni za 
Bunge Maalum za Mwaka 2014.

Hivyo, bila ya kuadhiri shughuli nyingine zitakazopangwa na Bunge, leo tarehe 13 Machi, 2014 saa 10.00 Jioni, Wagombea wafuatao watapigiwa kura:-

  1. Ndg. Amina Abdallah Amour; na
  2. Ndg. Samia Suluhu Hassan.
Tunapenda kutoa shukrani kwa Wagombea wote kwa ushirikiano wao katika kukamilisha zoezi la uteuzi. Aidha, tunaomba wapiga kura, wakati utakapofika, wazingatie matakwa ya Sheria na Kanuni zinazotawala uchaguzi huu.

Dkt. Thomas D. Kashililah 
KATIBU WA BUNGE 

Yahya Khamis Hamad
KATIBU WA BARAZA

WASIMAMIZI WA UCHAGUZI
13 Machi, 2014

------

Jioni ya leo mwendo wa saa 12 kasoro hivi, baada ya zoezi la kupiga kura kufanyika, Msimamizi wa uchaguzi alitamka kuwa kura zilizopigwa jumla zilikuwa 523. Kati ya hizo, kura zilizoharibika ni 7 (1.3%) wakati

  • Amina Abdallah Amour akipata kura 126 (24.1%) na
  • Samia Suluhu Hassan akipata 390 (74.6%)
Baada ya Msimamizi wa uchauguzi huo kusoma matokeo hayo, Mwenyekiti wa Muda wa Bunge, Mhe. Pandu Ameir Kificho aliwapa nafasi wahusika kutoa shukurani zao. 

Hatimaye, Mhe. Kificho alitangaza kuwa Makatibu wa Bunge hilo Maalumu tayari wameshaandaa orodha ya utaratibu wa namna ya kuapishwa kwa Spika na Makamu Mwenyekiti wake, zoezi ambalo limepangwa kufanyika hapo kesho.

Kikao kilifungwa kwa dua na kuahirishwa hadi kesho.

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

Share this :

Related Posts

0 Comments