Baada ya kupatikana maoni hayo baadhi yetu ama kwa kutokufurahishwa na matokeo ya maoni yenyewe ama kwa makusudi ya kutaka kupotosha ukweli wakaamua kuuita tume hii ni ya Jaji Warioba wala haiwataji watu maarufu wengine waliokuwa kwenye tume hiyo. Warioba siye aliyeunda tume ile bali rais wa tanzania. Nataka tuliweke sawa hili kwa manufaa ya watoto wetu.
Nashangaa hata aliyeiunda hakemei upotoshaji huu. Ripoti iliyosomwa na Warioba bungeni ni ripoti ya tume ya rais na ndiyo sababu hata ilipomaliza kazi walimpelekea ripoti ile mwenye kazi yake. Naye akibariki iende mbele kwa kuridhika na yaliyomo ndani ya ripoti. Labda naye mwenye kazi yake hajafurahishwa na maoni yaliyopatikana ndiyo sababu ananyamaza anapoona upotoshaji huu. Lakini siamini kuwa hakuridhika na ripoti ya tume kwani angweza kunyamaza kimya baada ya kuipokea na jambo lenyewe likaishia hapo kana kwamba hapakuwa na kitu. Hii isingekuwa mara ya kwanza katika historia ya nchi yetu kwani imepata kutokea hata kwa watangulizi wa rais huyu wa sasa. Kumbukumbu zinaonyesha Warioba aliwahi kuteuliwa kuwa mwenyekiti wa tume ya kuchunguza mianya na vyanzo vya rushwa na maeneo yaliyokithiri ili alete suluhisho la tatizo hilo. Mwenye tume alipopewa ripoti akaifungia na hakuna aliyewahi kuhoji hadi leo.
Kwa maana hiyo nathubutu kusema ripoti hii ya Tume ya kutengeneza katiba ilimfurahisha mwenye ripoti kwa kiasi kikubwa.
Eneo la pili ninalotaka tusaidiane kusahihisha ni maneno haya: "Tume ya marekebisho ya katiba au Tume ya kuunda/kutengeneza katiba mpya" lipi ni sahihi kwa tume hii? Kama ni tume ya marekebisho ya katiba maana yake ni kwamba ilitakiwa kufanya kazi ya kuondoa, kuingiza na kusahihisha baadhi tu ya maeneo yaliyomo kwenye katiba ya sasa kwa hiyo walichofanya si sahihi, lakini kama ni tume ya kuunda katiba mpya basi walichofanya ni sahihi.
Tafadhali wananchi wenzangu tusaidiane katika hili.
Kipamila
--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.
0 Comments