[Mabadiliko] michango katika jukwaa

Wednesday, January 22, 2014
Mimi nadhani kwa mfano: kusema kwa maana ya kutoa maoni kwa level yako kuhusu Zitto ni demokrasia sio uhafidhina hivyo sio kitu kikubwa kwa Mwenyekiti kuchukua sabbatical leave. 

Lakini nadhani pia dunia imeshakimbia mno kiasi kwamba matumizi ya hela ya Lowassa yanaweza kuonekana hayana madhara kwa taifa lakini ni hatari kwa watoto wetu

Mitandao ya kijamii inataka uhuru wa kujadiliana lakini isiyovuka mipaka kama ile ya mpuuzi Hamis Hamadi kutukana watu matusi yasiyofaa hata mbele ya wahuni wastaarabu. Nilitegemea Mwenyekiti aguswe zaidi na hulka hizo za members ambazo zinalipa jukwa siha fulani na sio kuhusu maoni ya members kuhusu watu fulani

Pamoja na yote haya na mengineyo, nadhani mawasiliano ni muhimu kuliko majaribio ya teknolojia. Kuzuia mawasiliano ya watu zaidi ya 1000 kwa kisingizio cha forum imeonyesha namna wote tusivyo na lengo la kweli la mabadiliko

Abdul

On Wednesday, January 22, 2014, Shigela Aloyce <comrshigela@gmail.com> wrote:

Kundi, na huo ndio uhuru wa mawazo na kunena. Vinginevyo kila tukiandikacho inatabidi kipitiwe na "wataalam", siyo?

SA.

On Jan 22, 2014 9:41 PM, "Godfrey Kundi" <gjkundi@gmail.com> wrote:
Bariki, kwani kuna tatizo gani katika kuponda au kusifia kama kuponda huko au kusifia huko kunaendana na hoja jadidi za Mpondo au Sifa hizo?

Nafikiri issue ya msingi ni kujenga hoja, na katika muktadha huo, hoja inaweza ikawa KWANINI Waziri wa NISHATI hatufai au anafaa, na nikajenga hoja za kumsifia kwa kufaa kwake au kumponda kwa kutofaa kwake.



2014/1/22 Leila Sheikh <calabashtz88@yahoo.com>
Yeeeeh!

 ----------
Sent from my Nokia phone

------Original message------
From: Richard Mabala <rmabala@gmail.com>
To: "mabadilikotanzania" <mabadilikotanzania@googlegroups.com>
Date: Wednesday, January 22, 2014 7:37:38 AM GMT-0800
Subject: [Mabadiliko] michango katika jukwaa

Waheshimiwa na waishiwa,
Baada ya kurudisha g mail, kwanza nawatakieni heri ya mwaka mpya kabla
mwaka haujachakaa kama mimi. Tudumu humuhumu kwenye mabadiliko na na
kuendeleza mabadiliko chanya kwa faida ya jamii na nchi yetu.

Aidha sina budi kukiri (hasa kwa wale walio wengi ambao wala hawakutambua
kwamba mwenyekiti hajaonekana ha ha) kwamba nilichukua likizo kidogo ya
Mabadiliko si kwa sababu ya U-BBC wangu (Born before Computers) maana
nimeweza kuingia kwenye wavuti mpya, bali kwa kuwa nilitaka kukaa na
kutafakari kidogo kuhusu mwelekeo wa Mabadiliko.

Naendelea kukiri kwamba niliamua kupumzika kwa sababu nilianza kujisikia
vibaya kuhusu baadhi ya michango na mijadala.  Mimi binafsi, na nakiri pia
kwamba yawezekana ni kutokana na mtazamo wangu finyu, sivutiwi hata kidogo
na hukumu bila uchambuzi.  Kwa mfano, baada ya Zitto kusimamishwa na chama
chake nikaona michango mingi mifupimifupi ya kumlaani, msaliti, haini, mla
rushwa n.k wakati upande wa pili bado kuna maswali hayajajibiwa hadi leo.
Inawezekana kweli yuko hivyo mimi sijui na nilitegemea kwamba wafuasi wa
chama ambacho mimi ningependa kishike madaraka watumie uchambuzi wa kina
zaidi siyo kushtumu tu.

Vivyo hivyo upande wa Lowassa.  Fisadi yule, atakiona mwaka 2015.  Lakini
nikiangalia pamoja na ufisadi wake anajua siasa na wakati wanamabadiliko
tunamdismiss anaendelea kujijenga, si tu kwa kutoa pesa bali kwa kuongelea
mambo ya sera.  Siwezi kumsameha kwa jinsi alivyobomoa elimu ya sekondari
kwa shule zake za ukata, na sikubaliani na siasa yake ya maamuzi magumu
bila maamuzi sahihi lakini ukweli ni kwamba naamini tunamdismiss at our
peril.  Tunapenda mabadiliko ndiyo lakini tumefanya nini kumneutralise
Lowassa, au Kinana au wengine.  Haitoshi kumlaani.  Wapi mikakati ya
kuwashughulikia.  Hasa upande wetu wanamabadiliko lazima iwe kwa hoja siyo
laana tu.

Na vivyo hivyo kwa wengine pia.  Mimi namheshimu Winnie Mandela kupita
kiasi lakini siko tayari kumdismiss Graca Machel ambaye naye amefanya mengi
makubwa na mazuri.  Kuna haki gani kuona kwamba kazi yake ni kuwasaka
marais tu.

Najua mambo mengine ni utani lakini lazima niseme kwamba hii twitter style
ya kuwadismiss watu kwa mstari mmojamoja unanikera kupita kiasi.  Huenda ni
udhaifu wangu au hata uBBC wangu.  Labda wakati wa mapambano inabidi
kuwadismiss na kuwahukumu watu bila kuwashinda kwa hoja sijui, labda nakuwa
too academic, lakini nilitegemea uchambuzi zaidi.   Niliachana na wanabidii
kutokana na udikteta wa mwenye jukwa na siwezi kurudi pale k(kama vile
political correctness) wa sababu hiyohiyo lakini naona kuna kama aina ya
mabadiliko correctness ambayo ni kuwadismiss wasiokubaliana na sisi.
Siafiki hii hata kidogo.

Nakaribisha maoni yenu.  Inawezekana na makengeza yangu yananisumbua.
Lakini katika maazimio yangu ya mwaka 2014 baada ya kutafakari kwa muda,
nimeamua nisiogope kutwitterika na mimi kwa sababu sikubaliani nao.

Tuwe na mwaka wa mabadiliko ya kweli yanayojengwa juu ya misingi imara, na
vitendo lukuki.
Mabala

--
Unapokea Email hizi kwa sababu umejiunga na Jukwaa la 'Mabadiliko'.
Kuchangia mada tuma kwenye Email hii: mabadilikotanzania@google

--
Unapokea Email hizi kwa sababu umejiunga na Jukwaa la 'Mabadiliko'.
Kuchangia mada tuma kwenye Email hii: mabadilikotanzania@googlegroups.com
 
MUHIMU KWA WANACHAMA WOTE: Jukwaa hili litafungwa hivi karibuni hivyo hii ni taarifa ya Mwisho kwako kuhakikisha unajisajili www.mabadiliko.com
 
For more options, visit this group at:
http://groups.google.com/group/mabadilikotanzania?hl=en?hl=en
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Mabadiliko Forum" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to mabadilikotanzania+unsubscribe@googlegroups.com.
To post to this group, send email to mabadilikotanzania@googlegroups.com.
Visit this group at http://groups.google.com/group/mabadilikotanzania.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.

Share this :

Previous
Next Post »
0 Comments