[wanabidii] Taarifa ya Kamati ya PAC baada ya kukutana na BoT

Monday, March 17, 2014
Kamati ya PAC Leo imekutana na Benki Kuu ya Tanzania kupokea Maelezo kuhusu fedha Tshs 201 bilioni za akaunti ya Tegeta Escrow. Fedha hizi zinahusiana na mkataba IPTL. PAC ina wasiwasi kwamba TANESCO, kwa mujibu wa nyaraka, itatakiwa kulipa fedha nyingi zaidi zinazofikia zaidi ya Tshs 200 bilioni kwa kampuni iliyonunua IPTL.

Kamati imeamua kwamba:-
  1. Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali afanya ukaguzi maalumu wa suala zima IPTL na uhalali wa utoaji wa fedha kutoka akaunti maalumu ya tegeta escrow.
  2. TAKUKURU waanze uchunguzi wa mchakato mzima wa mkataba wa IPTL, umiliki wa kampuni hiyo na uhamishaji wa umiliki kwenda kampuni ya PAP.
Kamati imeshangazwa na kitendo cha Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini kuanzisha 
ukaguzi maalumu wakati yeye mwenyewe ni mtia saini kwenye hati ya kutoa fedha hizo na mshiriki mkubwa katika mchakato mzima. Hivyo, kamati imeagiza ukaguzi maalumu kutoka kamati PAC ili kuweza kupata ukweli.

PAC imetoa mpaka mwisho wa mwezi Aprili kwa taarifa ya ukaguzi huo kuwa umekamilika na kuwataka wahusika wote wa mchakato wa IPTL kusubiri matokeo ya ukaguzi.

PAC imetaka pia maamuzi ya mahakama kuheshimiwa.

Imetolewa na 

Mwenyekiti PAC-Zitto Kabwe(MB)
Dodoma
Jumapili 16 Mechi 2014

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

Share this :

Previous
Next Post »
0 Comments