[wanabidii] Nyaraka nyeti zinazozungumzia utawala wa Sultan wa Oman na Zanzibar , zimeibwa

Monday, March 03, 2014
Nyaraka nyeti zinazozungumzia utawala wa Sultan wa Oman na Zanzibar kabla ya Mapinduzi ya Mwaka 1964, zimeibwa na watu wasiojulikana huko Zanzibar.


Taarifa zinaeleza kwamba nyaraka hizo zimeibwa katika Wizara ya Nchi Ofisi ya Rais Kazi na Utumishi wa Umma.

Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Katiba, Sheria na Utawala Bora wa Baraza la Wawakilishi, Ussi Jecha Simai ametoa taarifa hizo Leo wakati akiwasilisha ripoti ya kamati hiyo katika mwaka Fedha 2013/14 kwenye kikao cha <em>Baraza la Wawakilishi </em>kinachoendelea huko Chukwani mjini Unguja.

Kutokana na kuibwa kwa nyaraka hizo, vyombo vya usalama vya Zanzibar, vimeagizwa kuhakikisha wanachunguza na kubaini watu waliohusika kuiba nyaraka hizo muhimu za Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.

Share this :

Related Posts

0 Comments