Habari zenu,
Maendeleo ya nchi yetu pamoja na mambo mengine, yatatokana sana na uongozi. Lakini kwa mujibu wa katiba yetu, wananchi ndio wenye wajibu wa kuchagua miongoni mwa wagombea walio simamishwa na vyama vyao vya siasa na kuwafanya kuwa viongozi.
Kwa hiyo ni wazi kama Watanzania tuna kila sababu ya kuhoji utendaji kazi wa vyama hivi vya siasa ili kupima uwezo wa wanasiasa wetu ambo kwa namna moja ama nyingine ndio watakao ongoza nchi yetu na raslimali zake.
Kwa kutambua uwepo wa CHADEMA kama chama kilichojizolea umaarufu mkubwa kwa kipindi kifupi na matumaini ya Watanzania. Ningependa mjadala wangu ujikite zaidi ndani ya CDM haswa kwa kujadili yale mafanikio na mapungufu ya Dr Slaa.
MAFANIKIO YA DR SLAA TANGU AWE KATIBU MKUU CHADEMA.
1. Dr Slaa ameweza kukijenga zaidi CHADEMA na kukifikisha vijijini. Katika uongozi wake Dr Slaa ndipo niliona kuzinduliwa kwa operesheni kama vile M4C, operesheni okoa kusini na operesheni sangara.
2. Dr Slaa ameweza kufanya chama kupata raslimali za kufanyia kazi. Nimeshuhudia katika uongozi wake CDM ikipata magari, bodaboda na vitu vingine vya uenezi wa chama.
3. Kwa mujibu wa makatibu uenezi wa CDM wanadai chini ya uongozi wa Dr Slaa chama kiliweza kujipatia wanachama maradufu kulinganisha na wanachama wao kabla DR ajakamata uskani.
Kwa maono yangu haya ndio mambo ambayo nimesikia na baadhi kushuhudia kama mafanikio ya Dr Slaa kama katibu mkuu wa CHADEMA.
KUSHINDWA KWA DR SLAA KAMA KATIBU MKUU, CHADEMA.
Yafuatayo ni mambo ambayo yana dhihirisha kuwa Dr Slaa ameshindwa kuongoza chama katika nafasi yake aliyonayo:
1. Kushindwa kuondoa upendeleo wa ukabila na ukanda uliokithiri ndani ya chama anacho kiongoza. Hapa tumeshuhudia wagombea wengi ndani ya CHADEMA ni wale wenye mahusiano na kikanda au kinasaba na viongozi wa CHADEMA.
2. Kushindwa kudhibiti matumizi ya anasa CHADEMA. Mishahara na posho ni kubwa mno kwa chama cha wazalendo kama CDM.
Kuna taarifa zinasema Dr Slaa analipwa sawa na stahiki za wabunge wakati kila siku Watanzania tunalia kwa wabunge kupewa pesa nyingi za walipa kodi.
3. Kupoteza mvuto ambao tayari ulikuwepo CHADEMA na kupelekea CHADEMA kushindwa vibaya kwenye uchaguzi wa kata 27 na kufanya waambulie kata 3 tu.
4. Kubariki hali ya fujo, migogoro na ugomvi ndani ya chama kwa kuruhusu viongozi wa chama kurushiana maneno kwenye mitandao ya kijamii bila ya yeye kama kiongozi wao kuchukua hatua stahiki.
5. Kushindwa kulinda maadili ya kiungozi na kuruhusu media kumchezea kama zinavyo taka. Itakumbukwa sakata lake na Josephine lilivyo mdharirisha na kupelekea Watanzania kuichukia CDM.
6. Dr Slaa ana weakness ya kuwa jeuri, king'ang'aniza na asiye ambilika. Yeye uwa ana simama na misimamo yake hata kama ni hasi na yenye madhara. Hii inatia hofu kama kweli mtu wa aina hii ataweza kuwa rais. Maana rais uendesha kazi zake kwa misingi ya kushauriwa.
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.
0 Comments