Denis
Naituma kama tulivyojadiliana. Huu ndiyo msimamo. Chapa na sambaza, tuwa-pre empty.
Milton Mahanga
CHANGAMOTO KWA MWENYEKITI BUNGE MAALUM SAMUEL SITTA
(Gazeti la Mtanzania limefanya mahojiano na mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba, Dr. Makongoro Mahanga ambaye amebainisha changamoto kubwa iliyojificha mpaka sasa inayomkabili Mwenyekiti wa Bunge hilo Samwel Sitta. Yafuatayo ni mahojiano kati ya mwandishi wa gazeti hili na Dr. Mahanga)
SWALI: Wewe ni mmoja wa wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba. Umepokeaje kuchaguliwa kwa Mhe. Samuel Sitta kuwa Mwenyekiti wa Bunge Maalum, na ni changamoto gani unazoona anakabiliana nazo katika kuendesha Bunge hili?
JIBU: Kwanza nampongeza Mheshimiwa Samuel Sitta na Mheshimiwa Samia Sululu Hassan kwa kuchaguliwa kuwa Mwenyekiti na Makamu Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba. Sina wasiwasi hata kidogo kuhusu uzoefu na uwezo wao wa kuongoza vizuri Bunge hili. Hata hivyo changamoto kubwa ninayoiona kwa viongozi wetu hawa na wengine watakaochaguliwa kuwa wenyeviti wa Kamati mbalimbali ni mtihani mkubwa sana walio nao katika siku zao za awali tu kama Kamati ya Uongozi katika kuhakikisha kwamba kazi ya Bunge Maalum ya kutengeneza Katiba inafanikiwa bila kukwama katika siku za mwanzo tu za kazi hii.
Nalisema hili kwa sababu kwa bahati mbaya au nzuri Kanuni ya 32(1) ya Bunge Maalum haikuelekeza utaratibu wa Kamati ya Uongozi kugawanya sura mbili mbili za kupelekwa kwenye Kamati mbalimbali kwa ajili ya kujadiliwa. Suala hili limeachiwa Kamati ya Uongozi
1
kutumia busara zake. Kwa mawazo yangu, huu ni mtihani mkubwa sana kwa Kamati ya Uongozi na inabidi kweli wajumbe wa Kamati hii watumie busara kubwa katika kuamua Sura za Rasimu ya Katiba za kuanza kupeleka kwenye Kamati mbalimbali kwa ajili ya kujadiliwa.
SWALI: Kwa nini unasema hivyo?
JIBU: Kazi hii ni ngumu kutokana na ukweli kwamba Tume ya Marekebisho ya Katiba chini ya Jaji Joseph Waryoba ilifanya kosa kubwa la kujadili na kupendekeza kuhusu michakato miwili ambayo kwa kawaida haiwezi kujadiliwa kwa pamoja. Duniani kote ambako Katiba ya nchi zinazotaka kuungana au zinazotaka kubadilisha muundo uliopo wa muungano wao, lazima mchakato wa kuamua Muundo na ule wa kuandaa Katiba ifanyike kwa hatua mbili tofauti bila kuchanganywa:
(1) Kwanza lazima Mwafaka upatikane kuhusu Muundo mpya unaotakiwa na wananchi wa nchi hiyo. Kama ni Muungano mpya, lazima Muundo wa Muungano ukubalike kwanza. Kama ni Muungano wa zamani (kama wa kwetu), lazima kukubaliana kwanza kama Muundo unabaki ule ule au unabadilishwa.
(2) Baada ya Muundo huo mpya au uliobadilishwa kukubalika na Wananchi, au Chombo Mahsusi kama Bunge Maalum la Katiba, ndipo Mapendekezo ya Katiba itakayokidhi Muundo huo unaanza kuandaliwa na kujadiliwa na Bunge Maalum au na Chombo kitakachokubaliwa.
Hivi ndivyo hata wazee wetu, Mwalimu Nyerere na Abeid Karume na wenzao walivyofanya kwa kukubaliana kwanza kuhusu Muundo wa Serikali mbili (hii ilifanyika kwa Mkataba wa Muungano wa tarehe 22 Aprili 1964), na ndipo wakaagiza sasa Katiba iandaliwe ambayo ingekidhi hizo Serikali mbili (hii ilifanyika baadaye kwa Sheria ya Bunge ya Katiba ya Muda Na. 43 ya tarehe 10 Julai 1965). Uchambuzi unaonyesha kwamba nchi zote duniani, zenye muungano kama wa kwetu, ambazo ziliamua kubadili au kuhoji kuhusu Muundo wa Serikali uliopo, walifanya michakato hiyo kwa hatua tofauti (na sequencially) kwa kuanza mchakato
2
namba (1) hapo juu wa Muundo, na baada ya maridhiano kwenda sasa kwenye hatua ya pili ya kuandika Katiba itakayokidhi Muundo huo uliokwisha kubalika.
SWALI: Kwani Hadidu za Rejea za Tume ya Mabadiliko ya Katiba hazikuwataka kuangalia pia Muundo wa Muungano?
JIBU: Hapana. Inaonekana Tume ya Katiba haikuzingatia vyema hadidu zake za rejea. Ukipitia vizuri Sheria ya Mabadiliko ya Katiba ibara ya 9 na 17 zenye Hadidu za Rejea za Tume, na hata Tangazo la Serikali namba 110 ya mwaka 2012 ibara ya 4 (3), 18, 19 na 20 zinazofafanua hadidu hizo za rejea, suala la kushughulikia Muundo wa Muungano halikuwepo. Yaonekana kwamba Mamlaka iliyoiteua Tume iliamini kwamba Hadidu za Rejea kwa Tume zilikuwa wazi kwamba suala la Muundo mpya wa Muungano halikuwemo, isipokuwa kupendekeza Katiba itakayoweza kurekebisha, kuondoa na kuongeza vifungu vitakavyosaidia kuboresha Muundo tulionao kama Mkataba wa Muungano wa mwaka 1964 ulivyoeleza bayana. Kwa hiyo Tume ya Katiba iliamua tu kuongeza suala la Muundo wa Muungano kwenye hadidu rejea zake, na Mamlaka ya Uteuzi kwa bahati mbaya pia haikuweza kuzuia hatua hii kuendelea baada ya kuona Rasimu ya Kwanza.
SWALI: Dr. Mahanga, huoni kwamba inawezekana Tume baada ya kuanza kazi ya kuandaa Katiba Mpya na katika mahojiano na wananchi waliona kwamba suala hilo la Muundo wa Muungano linajitokeza sana na hivyo wakaamua kuliingiza kwenye hadidu rejea zake?
JIBU: Hata kama katika kazi yao ya kuandaa Rasimu ya Katiba Tume iligundua kwamba wananchi wengi walikuwa wanataka Muundo ubadilike, walitakiwa kurudi kwa aliyewateua ili kushauri kwamba mchakato wa kujadili na kuamua kubadilisha Muundo, au la, ufanyike kwanza ndipo hatua ya pili ya kuandaa Katiba inayokidhi Muundo utakaokubalika ufuate. Hawakufanya hivyo, wakachanganya michakato miwili hii kwa pamoja na hivyo kuzua malumbano makubwa sana ndani ya jamii ya watanzania wakati Rasimu yao ya Katiba ilipokuwa inajadiliwa. Hatua hiyo ilisababisha wananchi kushindwa kujadili vizuri mapendekezo ya Katiba wakabaki wanalumbana kuhusu Muundo wa Muungano zaidi, kazi ambayo ilitakiwa ianze kwanza kabla ya kujadili Katiba.
3
SWALI: Kwa kuwa unasema makosa yameshafanyika na Tume, kwa maoni yako sasa Mwenyekiti Sitta na Bunge Maalum mfanye nini kurekebisha hali hii?
JIBU: Ni kweli makosa yameshafanyika na Tume na inabidi sasa Bunge Maalum lijaribu kurekebisha makosa hayo. Njia ya wazi ya kurekebisha kasoro hii ni Bunge Maalum kugawa Rasimu hii ya Katiba katika michakato hiyo miwili iliyochanganywa na Tume, na kuanza kujadili na kukubaliana kwanza kuhusu Muundo, na baadaye ndipo lianze kujadili kuhusu Katiba itakayokidhi Muundo huo tutakaokuwa tumekubaliana kwenye Bunge Maalum. Ukiangalia Rasimu ya Katiba michakato hii miwili iliyochanganywa ni kama ifuatavyo:
1. Muundo wa Muungano (Sura ya Kwanza na Sura ya Sita)
2. Katiba ya Jamhuri ya Muungano (Sura 15 zilizobaki)
Kwa hiyo njia ya kwanza rahisi na ngumu kwa Mheshimiwa Sitta na Kamati yake ya Uongozi ni kuamua kutoa Sura ya Sita na Sura ya Kwanza (Muundo) ili zijadiliwe na kukubalika na Kamati za Bunge na hatimaye kupitishwa na Bunge Maalum, kabla ya kuendelea kugawa na kujadili sura zingine (Katiba).
SWALI: Kwa nini unasema njia hii ni rahisi na ngumu?
JIBU: Ni rahisi kwa sababu Bunge Maalum litakuwa limerekebisha kosa la Tume nililoeleza hapo juu kwa kutenganisha michakato ya kukubaliana kuhusu Muundo wa Muungano na Mchakato wa kuandaa sasa Katiba inayokidhi Muundo utakaokuwa umekubalika kama inavyofanyika duniani kote.
Lakini njia hii ni ngumu kwa sababu iko hofu kwamba hatua hii inaweza kusababisha Bunge la Katiba likavunjika mapema sana labda wiki moja tu baada ya kuanza kujadili Sura ya Sita na ya Kwanza. Hii ni kwa sababu suala la Muundo wa Muungano ndilo suala linaloonekana kubwa na zito zaidi katika Rasimu hii na wajumbe wa Bunge Maalum wamegawanyika sana kuhusu muundo wa Serikali mbili na Serikali tatu. Hofu iliyopo ni kwamba inawezekana ibara za sura hizi, hasa Sura ya Sita, zikakosa kupata theluthi mbili za kura za wajumbe kutoka pande zote za Muungano, hata kura zingepigwa mara tatu. Ingawa Kanuni 36(4) inaelekeza kwamba ibara
4
inayoshindwa kupata theluthi mbili ya kura toka kila upande wa Muungano itapelekwa kwenye Kamati ya Mashauriano, ibara za Sura ya Sita ni nyeti sana na sura na ibara nyingi sana za Rasimu zinategemea muafaka kupatikana kuhusu Sura ya Sita ya Muundo wa Muungano. Hivyo ibara za Sura ya Sita haziwezi kungojea ziamuliwe na Kamati ya Mashauriano huku wajumbe wakiendelea na Sura zingine. Bunge Maalum litakwama tu!
SWALI: Na njia ya pili ni ipi?
JIBU: Pengine busara ya Mwenyekiti Sitta na Kamati yake ya uongozi inaweza kuwatuma kuacha njia hii ya kwanza na kufuata njia ya pili: Kugawa kwanza kwenye Kamati mbalimbali zile Sura ambazo hata ikiwa ikiamuliwa Serikali mbili au tatu bado ibara na Sura hizo haziwezi kubadilika sana, na kuacha kwanza Sura zile ngumu kama Sura ya Sita na zingine zenye muelekeo wa kubadilika sana kutegemea na Muundo wa Muungano. Njia hii ya pili itafanya Bunge Maalum liendelee na kazi zake kwa muda fulani kwa mafanikio au makubaliano. Hata hivyo, bado Bunge litarudi tu kwenye Sura ya Sita na ya Kwanza kabla ya kujadili sura kama ya 7 (Serikali ya Jamhuri ya Muungano), Sura ya 8 (Uhusiano na Uratibu wa Serikali); Sura ya 9 (Bunge la Jamhuri ya Muungano); Sura ya 10 (Mahakama ya Jamhuri ya Muungano); Sura ya 12 (Uchaguzi Katika Vyombo vya Uwakilishi); Sura ya 14 (Masharti Kuhusu Fedha za Jamhuri ya Muungano), na Sura ya 15 (Ulinzi na Usalama wa Jamhuri ya Muungano). Bila kukwamua Sura ya 6 itakuwa vigumu kujadili hizi sura zingine saba nilizotaja hapo juu.
SWALI: Sasa una ushauri gani kwa Mwenyekiti Samuel Sitta na Kamati ya Uongozi?
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.
0 Comments