[Mabadiliko] Tuwe wakweli kwa nafsi zetu na nchi yetu; Ndoa yenye kero kwa miaka 50 inawezaje kuitwa ndoa...?

Tuesday, March 18, 2014

Ndugu zangu,

Kwamba hata wajuu wakue wazikute kero za ndoa ya bibi na babu yao. Hapo kuna tatizo kubwa. Na tatizo hilo litakuwa ni la kimfumo.

Tunapozungumzia suala la Muungano tunafanya makosa makubwa kufananisha na visivyostahiki kufananishwa. Sijapata bahati ya kumsikiliza Jaji Warioba leo, lakini, kwa kusoma hotuba ya maandishi, nauona upotoshwaji wa makusudi na pengine kuwabeza wale wenye hoja ya uwepo wa Muungano wa Mfumo wa Shirikisho la Serikali Tatu.

Lakini huko hakutusaidii kupata jawabu la suala la mfumo wa Muungano, badala yake ni kushusha kiwango cha mijadala na hata kupelekea kuvunjika kwa Muungano wenyewe.

Kwa kusoma hotuba ya Warioba, na kwa mtu yeyote mwenye tafakuri pevu hawezi kuaminishwa kirahisi kuwa Warioba na wenzake kwenye Tume ya Katiba, akina Jaji Augustino Ramadhan, Dr . Salim Ahmed Salim, Joseph Butiku na wengineo, kuwa wanayo dhamira ya kuuvunja muungano wetu.

Ni vema tukakubali na kuwaamini, kuwa wana dhamira ya dhati ya kuulinda na kuuimarisha Muungano wetu katika mfumo walioupendekeza kwetu ambao kimsingi umetokana na mawazo ya sisi wananchi wenyewe. Na kutetea aina nyingine ya mfumo wa Muungano, nao watuwekee mezani hoja zao tukazishindanisha. Yumkini zaweza pia kutushawishi.

Ndugu zangu,

Hili la Katiba lisitufanye tukawekana katika makundi, kwamba wengine ni maadui wa umma na wengine ni wazalendo zaidi.

Na mwisho wa siku, ni muhimu kwa viongozi na wananchi kwa ujumla wetu, kuwa tukajiandaa kwa kile ambacho kitaamuliwa na wananchi na ambacho wananchi wenyewe wanajua kama ni chenye kuwafaa na wana maslahi nacho.

Hii ni Nchi yetu sote. Tufanye na tuseme yenye kutanguliza hekima na busara ili tubaki kuwa wamoja na wenye kuheshimiana.

Jioni Njema.

Maggid Mjengwa,
0754 678 252
http://mjengwablog.com

--
Unapokea Email hizi kwa sababu umejiunga na Jukwaa la ‘Mabadiliko’.
Kuchangia mada tuma kwenye Email hii: mabadilikotanzania@googlegroups.com
 
 
For more options, visit this group at:
http://groups.google.com/group/mabadilikotanzania?hl=en?hl=en
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Mabadiliko Forum" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to mabadilikotanzania+unsubscribe@googlegroups.com.
To post to this group, send email to mabadilikotanzania@googlegroups.com.
Visit this group at http://groups.google.com/group/mabadilikotanzania.
To view this discussion on the web visit https://groups.google.com/d/msgid/mabadilikotanzania/CAMD-ye47wWvXxeydNq%2B1ip9szQBan4N2Dv1mtciY7Jz7rDwQwA%40mail.gmail.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

Share this :

Previous
Next Post »
0 Comments