[Mabadiliko] Hongera Rais Kikwete kwa hotuba nzuri ...

Friday, March 21, 2014
Nachukua nafasi hii kumpongeza Mhe. Rais Jakaya Mrisho Kikwete kwa hotuba nzuri na iliyojaa hekima na busara kwenye uzinduzi wa Bunge maalumu la Katiba.

Kimsingi amewataka wajumbe kuwa makini na kutafakari kila kifungu cha rasimu ya katiba ili watuletee katiba bora itakayoweza kutekelezeka.

Kuhusu muundo wa Serikali amesema tuna uwezo wa kufanya mabadiliko yoyote bila kuhitaji 3.

Watanzania tuna haja ya kutafakari kwa kina na kuamua mustakabali wa nchi yetu.

Mimi ni muumini wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, naamimi kabisa tuna uwezo wa kupambana na changamoto zote zinazojitokeza bila kuongeza gharama za uendeshaji wa serikali yetu kwa kuunda Serikali ya 3.

Tujiulize yaliyowakuta wenzetu Warusi baada ya kuunda Serikali ya Russia, Muungano wao wa USSR ulivunjika na sasa wanatumia gharama nyingi kurudisha shirikiksho hilo na kuzishikilia baadhi ya nchi hizo.

Tutafakari na tufanye maamuzi kwa faida ya Taifa letu, tuachane na hisia za utaifa wa Utanganyika na Uzanzibari madhara yake ni makubwa na tutangeneza dhambi na adhabu yake tutaipata hapa hapa.

Mungu ibariki Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Phares Magesa.



Sent from my BlackBerry(R) smartphone provided by Airtel Tanzania.

--
Unapokea Email hizi kwa sababu umejiunga na Jukwaa la 'Mabadiliko'.
Kuchangia mada tuma kwenye Email hii: mabadilikotanzania@googlegroups.com


For more options, visit this group at:
http://groups.google.com/group/mabadilikotanzania?hl=en?hl=en
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Mabadiliko Forum" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to mabadilikotanzania+unsubscribe@googlegroups.com.
To post to this group, send email to mabadilikotanzania@googlegroups.com.
Visit this group at http://groups.google.com/group/mabadilikotanzania.
To view this discussion on the web visit https://groups.google.com/d/msgid/mabadilikotanzania/BLU0-SMTP2579C6A5327FC113C95510CD3790%40phx.gbl.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

Share this :

Related Posts

0 Comments