A. Mapendekezo ya Rasimu ya Katiba
Rasimu ya katiba imependekeza katiba ibara 98(2) idadi ya mawaziri na manaibu waziri isizidi 15. Ibara 67(1) inapendekeza uwepo wa mawaziri wakazi mmoja toka kila upande watakaoratibu mambo ya muungano kwa serikari zao. Ikapendekeza uwepo wa waziri mwandamizi ambaye kimsingi ni waziri mkuu katika ibara 99(1). Ikapendekeza pia katiba ibara 105(1) uwepo wa katibu mkuu kiongozi. Pia imependekeza kuundwa kwa tume ya uhusiano na uratibu wa serikali.
B. Wizara zitakazotokana na mambo ya Muungano. Kwa mambo ya muungano rejea rasimu ya katiba ibara 63 au ukurasa wa mwisho wa rasimu ya katiba.
1. Wizara ya Katiba na Sheria.
2. Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa. (JWTZ na JKT)
3. Wizara ya Mambo ya Ndani (Uhamiaji , Polisi na FFU )
4. Wizara ya Fedha na Uchumi (sarafu, benki kuu na mamlaka ya mapato)
5. Wizara ya Mambo ya Nje.
C. Jumla ya Mawaziri Kwa mujibu wa Rasimu
Kutakuwepo mawaziri na manaibu waziri 10 watakaotokana na mambo ya muungano, Mawaziri Wakazi wawili na Waziri Mwanamizi wa muungano (rejea kipengele A ). Hii itafanya Jumla ya Mawaziri na Manaibu Waziri kuwa 14 na ukiongeza mwanasheria mkuu wa serikali kwasababu anakuwa na uzito wa waziri.
D. Mapendekezo yangu ya Wizara za Muungano
1. Wizara ya Sheria na Haki (Polisi wa shirikisho, Idara ya Upelelezi ya Taifa).
2. Wizara ya Ulinzi (JWTZ na JKT)
3. Wizara ya Mambo ya Ndani (Uhamiaji, Mamlaka Viwanja vya Ndege na Bandari, Usalama wa Taifa).
4. Wizara ya Uchumi na Fedha (TRA, Benki Kuu, Sarafu ).
5. Mambo ya Nje
6. Wizara ya Maliasili na Utalii
7. Wizara ya Nishati.
8. Wizara ya Kilimo na Chakula.
9. Wizara ya Biashara na Viwanda
10. Wizara ya Kazi na Ajira.
11. Wizara ya Afya
12. Wizara ya Elimu.
E. Muundo wa Serikali kwa mujibu wa Mapendekezo yangu.
1. Hakutakuwa na Waziri Mwandamizi (Waziri Mkuu) kwani shughuli zake zinaweza kufanywa na Katibu Mkuu Kiongozi (KMK) wa Ikulu (Chief of staff )ambaye ni mtu wa karibu na Rais. Hivyo KMK atachaguliwa na rais na hatopitishwa bunge au chombo chochote cha usaili. The bucks stops with president msemo unaotumika na jamhuri nyingi zisizo na middlemani (Waziri Mkuu); msalaba anabeba Rais mwenyewe.
2. Hakutakuwepo mawaziri wakazi kushughulikia mambo ya muungano wa serikali za washirika, pia hakutakuwepo tume ya uhusiano na uratibu wa serikali. Mitafaruku ya kimamlaka kati ya serikali zote tatu itaamliwa na mahakama kama viongozi wa serikali zote watashindwa kuwasiliana. Tunafanya mageuzi kwenye mfumo wa mahakama ili kutatua migogoro ya kikatiba kama hiyo. Hatuitaji mawaziri wakazi wawili kukaa wakisubiri migogoro kwani kila serikali itakuwa na mshauri wa kisheria atakayeishauri serikali yake kabla ya kutekeleza suala lolote kuangalia kama halitaleta mgongano wa kimamlaka.
3. Hakutakuwa na manaibu waziri, kila wizara itakuwa na waziri kamili mmoja. Katika kila wizara uwa kunakuwa na idara mbalimbali, hivyo wakuu wa hizo idara kwa usawa watakuwa wasaidizi wa waziri wao (assistant to the minister) mbali na uwepo wa katibu mkuu wa wizara.
4. Hakutakuwa na wizara ya sheria na mambo ya katiba badala yake kutakuwepo wizara ya sheria na haki itakayokuwa chini ya mwanasheria mkuu wa serikali. Wakuu wa idara kwa usawa watakuwa wasaidizi wa mwanasheria mkuu, mfano mkuu wa TAKUKURU au mkuu wa kudhibiti magendo, nk. (Rejea muundo wa serikali ya Kenya na Marekani).
5. Hivyo kwa mujibu wa vipengele 1, 2, 3 na 4; kutakuwa na wizara 12 ninazopendekeza zenye jumla ya mawaziri 12. Nyingine zitabaki kama idara za kawaida zenye wakuu wanaomshauri rais moja kwa moja mfano mkuu wa idara ya usalama wa taifa (au mtu atayekuwa amepangwa) atalazimika kumpa taarifa rais kila siku juu ya hali ya kiusalama ya taifa.
6. Katika mapendekezo yangu nimeongeza wizara 7 ambazo nimeona ni muhimu kama taifa kuwa na sera ya pamoja. Wizara ya maliasili na utalii: kama taifa tunahitaji kuwa na sera ya pamoja ya uhifadhi maliasili kwa vizazi vijavyo. Wizara ya Kilimo na Chakula: lazima taifa liwe na mipango ya upatikanaji wa chakula kwa raia wake, hivyo sera ya kilimo ya pamoja ni muhimu. Wizara ya Nishati: lazima taifa liwe na sera moja ya nishaji ili kuhakikisha tuna nishati ya kutosha kwani ili taifa kuendelea linahitaji nishati. Wizara ya Biashara na Viwanda: Lazima tuwe na sera ya utafutaji masoko na biashara kwa bidhaa za ndani kwenda nje. Wizara ya Kazi: itakayoweka mipango jinsi ya kuongeza ajira na kufuatilia mwenendo wa hali ya ajira nchi.
HITIMISHO:
Rasimu ya katiba, muundo wa serikali ni wa kasumba ya zamani ya kuweka wizara na tume zisizo za lazima kama wizara ya muungano chini ya mawaziri wakazi., waziri mwandamizi, nk. Yote haya yanaongeza gharama za bure. Mapendekezo yangu ni sawa tu na mataifa mengi yenye mfumo wa shirikisho iwe jamhuri au ufalme.
Mfano Ethiopia, Kenya, Afrika Kusini, Marekani, Australia hawana Waziri wa Katiba na sheria bali wizara iko chini ya Mwanasheria mkuu wa serikali. Kenya wameunda Wizara ya kuratibu majimbo lakini imeshindwa kutatua migogoro ya kimamlaka kati ya serikali kuu na majimbo 47 imebaki tu kushughulikia mgawanyo wa mapato kitu ambacho kingefanywa na mamlaka ya mapato kwa kanuni ya idadi ya watu. Magavana wamefungua kesi ya kikatiba mahakama ya juu.
Inawezekana kuna watu wanafikiri Serikali ya muungano itakuwa na mikoa na wilaya: hapana mambo ya serikali za mitaa yako chini ya serikali za washirika, wanaweza kuamua kuongeza au kupunguza mikoa iliyopo sasa kulingana na vipaumbele vyao na mapato wanayopata.
Serikali za washirika zinaweza kuwa na wizara ndogo zaidi au sawa na wizara za shirikisho kwani Serikali ya Tanganyika au Zanzibar haziwezi kuwa na wizara ya mambo ya nje, wizara ya ulinzi na mambo ya ndani. Zinaweza kuwa na idara za usalama wa raia wa majimbo.
BUNGE: Bunge la Muungano litakuwa dogo hivyo tunategemea na mabunge ya washiria yawe madogo.
Kiujumla gharama za shirikisho ni ndogo sana kuliko ilivyo sasa chini ya serikali moja yote kutokana na mgawanyo wa majukumu.
Tukiamua kufuata mapendekezo ya tume na tusiwe na manaibu waziri basi serikali ya shirikisho itakuwa ndogo zaidi kuliko hata mapendekezo yangu ingawa serikali za washirika zitakuwa na wizara nyingi kuliko shiriksho.
-- Rasimu ya katiba imependekeza katiba ibara 98(2) idadi ya mawaziri na manaibu waziri isizidi 15. Ibara 67(1) inapendekeza uwepo wa mawaziri wakazi mmoja toka kila upande watakaoratibu mambo ya muungano kwa serikari zao. Ikapendekeza uwepo wa waziri mwandamizi ambaye kimsingi ni waziri mkuu katika ibara 99(1). Ikapendekeza pia katiba ibara 105(1) uwepo wa katibu mkuu kiongozi. Pia imependekeza kuundwa kwa tume ya uhusiano na uratibu wa serikali.

Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.
0 Comments