[wanabidii] POSHO SH 300,000 KWA SIKU HAITOSHI!

Friday, February 21, 2014
Ama kweli, ule usemi usemwao, mkuki kwa nguruwe.... umetimia. Ni kilio cha muda mrefu kwa watanzania kima cha chini cha mshahara walao kiwe sh. 300,000 kwa mwezi. Inakataliwa na inasemwa haiwezekani.

Kumbe jamaa zetu wenye rungu hilo wanasema 300,000 kwa siku haiwezekani. Je na yule anayepata 150,000 kwa mwezi, mwenye mahitaji kama wewe. Ana familia, anakula, anavaa, anajenga, anasomesha, anaumwa, anasafiri, ana ndg wanaomtegemea. Wengine wameachiwa watoto Yatima au wajane WASEME NIN? 

FIKIRI NA MCHUKUE HATUA!

Share this :

Related Posts

0 Comments