[wanabidii] CCM inaimarika, CHADEMA inasinyaa, CUF inakufa

Wednesday, February 12, 2014
By Dr Kitila Mkumbo
Katika Makala Alioipost Jana Yenye Kichwa cha Habari’CCM is Stabilising, Chadema is Shrinking and CUF is Disappearing, Dr Kitila Mkumbo (Hon and Senior Lecture UDSM) Amesema Licha ya Chadema Kukubalika sana Mitaani na Kuwa na Mashabiki wengi LAKINI Chadema Haipati Kura za Kutosha Katika Chaguzi Kwa Sababu Kuu Nne:

1. Chadema Imeonekana Sio Mbadala Sahihi wa CCM (Chadema is not Credible Alternative of CCM).Licha ya Kwamba Chadema Imefanikiwa Kuweka wazi MABAYA ya CCM kwa Watanzania Lakini Imeshindwa Kuwashawishi Watu ya Kwamba wao ni Mbadala wa CCM.Dr Kitila Akaenda Mbali na Kusema ni Heri Kutawaliwa na Wakoloni Weusi (CCM) Kuliko Wakoloni WEKUNDU (Chadema) Maana hawa ni Zaidi ya Kudandia Meli ya Kigiriki.

2. Viongozi wa Chadema ni MAFISADI,Waroho wa Pesa na Viongozi Wenye Njaa Kali Kuliko Viongoozi wa CCM.Dr Kitila Amesema Viongozi wa Chadema Wanapenda Sana Posho Kuliko Viongozi wa CCM,Wanapenda Kutembelea Magari ya Kifahari sana Kuliko Viongozi wa CCM, Wanapenda Sana Safari za nje ya Nchi Ndio Maana Kila Siku Utasikia Freeman Mbowe na Mke wake Wameenda Kutalii Marekan,Dubai..kwa Pesa za Serikali.Kwa sababu hizo imekuwa ngumu kutofautisha Viongozi wa Chadema na wa CCM…

3. Chadema Hawataki KUKOSOLEWA na wala hawataki KUJILEKEBISHA:Dr Kitila Amesema,Ukiikosoa Chadema Hata Kama Unachokisema ni Kweli,Hawachelewi Kukuita wew ni MSALITI,Pandikizi la CCM,Umetumwa……na Mambo mengine ya Kiuchonganishi ili Wakuchafue Kisiasa.Hii ni Hatari sana kwa Chama Kichanga chenye Dhamila ya Kushika Dolla 

4. Mpasuko ndani ya Chadema:Dr Kitila Anasema,Viongozi wa Chadema Wametumia Muda mwingi wa kampeni kumchafua Zitto Kabwe na sio kuwanadi wagombea wao.Dr Kitila Amesema,Kitendo cha Chadema Kumtangaza Zitto Kabwe kama Muhaini wa Chadema na ili Hali wananchi wanajua Mchango wa Zitto katika mafanikio ya Chadema,Wananchi wamepoteza Imani kabisa na Chadema na Hawakitaki tena.

Dr Kitila Ameongezea kwamba:
Ni Bora Tuendelee Kutawaliwa na CCM Ambao Wanang’ata na Kupuliza Kuliko Hawa Viongozi wa Chadema Ambao wananjaa ya Kufa Mnyama.Hawa Wanaweza Kuiba Mpaka Tukaingia kwenye Vita ya Wenyewe kwa Wenyewe.
Dr Kitila Amemalizia kwa Kusem’Chama cha Upinzani Imara Bado Hakijazaliwa (A credible and Serious Opposition might be in the Offing) Hivyo Watanzania tuendelee kuwa na Subira na Vijana Tuache Kushabikia Chadema kwani Hakuna Chochote cha Ujenzi wa Taifa ndani ya Chadema Zaidi ya UOZO na WIZI....

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.

Share this :

Related Posts

0 Comments