[wanabidii] Kampuni za simu zinapopandisha gharama za 'simu' huwa inamaanisha nini?

Monday, January 27, 2014
Amani kwenu,

Hivi, napenda kufahamu, hizi kampuni za simu zinapopandisha gharama za wateja kupiga simu n.k huwa wanamaanisha nini? Yaani ni nini huwa kinawafanya wapandishe bei na siyo kupunguza?

Kwa mfano: Airtel kuna kifurushi hiki ya YATOSHA, kwa Tshs 2000 ulikuwa unaweza kupata Dk 60 za kupiga, ila wiki moja iliyopita kulitokea mabadiliko, kwa hiyo Tsh 2000 sasa unapata dk 40 badala ya 60, hapo ina maana wameongeza gharama. Sasa hivi hapa ni nini kimesababisha ongezeko hilo? Ni hii bili ya umeme iliyoongezeka? Ni kodi au ni kitu gani?

Pamoja na faida kubwa wanayopata hawa watu wa mtandao, ni ongezeko la gharama gani ambalo linaweza kuwa kubwa sana (kulinganisha na faida wanayopata) inayoweza kuwafanya wao kupandisha bei juu?

Kuna mtu anaweza kufahamu kuhusu hili?

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.

Share this :

Related Posts

0 Comments