[wanabidii] TUSIMUHUKUMU ZITTO KWA UKIGOMA

Monday, December 02, 2013
TUSIMUHUKUMU ZITTO KWA UKIGOMA. 

Napita kwenye mitandao naona inajengeka dhana ya kijinga kabisa kwamba mgogoro wa CHADEMA unaomuhusisha zitto unajadiliwa na baadhi ya watu kibaguzi na kwa dhana ya historia kwamba watu wa Kigoma wanapenda au ni waroho wa madaraka kwa kutoa mifano ya baadhi ya wanasiasa waliogombea kwenye vyama na kusababisha mvutano. Mimi niseme tu kwamba Kigoma ni sehemu ya Tanzania na watu wake wana haki zote za kugombea Kama wengine. Nachokijua kuhusu Kigoma ni mkoa wenye kupenda kuhoji na wasiopenda kabisa kubuluzwa au kufugwa akili. 

Ndio maana huu ndio mkoa pekee ambao ccm waliburuzwa vibaya..huu ni mkoa ambao ccm ni Chama cha upinzani kwani kina majimbo3 huku upinzani ukiwa na majimbo5. 

Hakuna mkoa mwingine uliochapa ccm Kama Kigoma. Ni mfano wa kuigwa na mikoa mingine Kama tunataka mabadiliko kweli. Tusihukumu mkoa kwa kutoa watu wanaopenda kugombea eti ni uroho wa madaraka, no! 
Mbona pale bungeni Kati ya vyama 5 upinzani vyenye wabunge vyama vitatu vinaongozwa na wenyeviti wenye asili ya mkoa mmoja wa Kilimanjaro ? Na hatusemi kwamba watu wa kilimanjaro ni waroho wa madaraka kwasababu kila mtu anajua alifikaje alipofika hivyo tusitake kujenga dhana ya watu Fulani hawastahili na watu Fulani wanastahili Bali tuangalie dhamira, upeo na uadilifu, basi. Na sifa hizo sio za kijiografia

CHANZO - DAVID KAFULILA 

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.

Share this :

Related Posts

0 Comments