Kwanza nianze kwa kuwaomba radha wanajamii, inawezekana ishu kama hii hili sio jukwaa lake lakini wahenga walisema palipo na wengi haliharibiki neno na pia post hii inaweza kusaidia pia watu wengine hapa jamvini.
Bila shaka humu kuna watu wenye watoto au uzoefu na malezi ya watoto. Nina mdogo wangu anamtoto wa miezi 8. Kwa kipindi kama cha miezi 2 iliyopita afya ya huyu mtoto imekua sio nzuri. Mara ya kwanza kabisa mtoto alikua anatapika kila chakula anachopewa.
walimpeleka dispensary ya jirani na makazi yao hapo wakampima wakasema ana malaria 2, wakampatia dawa na kumchoma sindano kuzuia kutapika. Mtoto alipata nafuu lakini baada ya muda kama wa wili 2 hivi ile hali ikajirudia. Walienda tena pale dispensary wakampima tena wakasema ana malaria 2 wakafanya kama awali ila safari hii walimbadilishia dawa. sasa hii hali imerudia kama mara 4 hivi na kila wakimpima wanasema ana malaria 2. Wamejitahidi nyumbani kuboresha mazingira ikiwa ni pamoja na kutumia dawa ya mbu, kumvalish nguo mwili mzima hasa jioni n.k bila mafanikio.
Wameniomba ushauri na baada ya kuwasikiliza nikahisi hii inaweza kuwa kuna tatizo lingine pia, baada ya hayo maelezo naomba tusaidiane maswali yafuatayo.
1) Ni hospital/Dispensary gani ambayo ni affordable lakini wanahuduma nzuri sana kwa uzoefu wako hasa mambo yanayosumbua watoto?
2) Kuna Dr yeyote wa watoto unayemfaham au hospital/Dispensary yake ambayo sio ghali sana anaweza kumpeleka huyu mtoto akachekiwe.
Ni hayo tu na samahani kwa usumbufu wowote
Natanguliza shukrani
0 Comments