[wanabidii] WATANZANIA NA HUJUMA DHIDI YA NCHI YAO

Wednesday, September 18, 2013

WATANZANIA NA HUJUMA DHIDI YA NCHI YAO  

Ndugu zangu ,

Imekuwa ni kawaida sana kwa baadhi yetu kutoa siri za nchi na baadhi ya maeneo kwa watu mbalimbali tunaokutana nao au tunapoulizwa kwenye makongamano huko nje ya nchi au hapa nchini haswa yale yanayoratibiwa na wafadhili .

Imekuwa ni kawaida kwa viongozi wa vyama haswa wa vyama vya upinzani kuita waandishi wa habari na kuwaeleza ubovu wa sekta mbalimbali haswa sekta za ulinzi na usalama kama jeshi la polisi na usalama wa taifa .

Imekuwa ni jambo la kawaida kwa baadhi yetu kurubuniwa na baadhi ya watu wanaojifanya marafiki/watalii kwenda kuwatembeza maeneo mbalimbali ya nchi huku wakipiga picha na kuchunguza mambo mbalimbali .

Imekuwa ni kawaida kwa ndugu zetu wakina dada kuolewa na jamaa wa nje na wakina kaka kuowa wadada wa nje wenye malengo ya kutumia uhusiano huo kuiba siri , kununua ardhi , kuwa karibu na baadhi ya watu haswa viongozi au kupata upenyo Fulani wa hujuma za muda mrefu dhidi yetu .

Ndugu zangu watanzania wenzangu tuwe makini na wimbi hili la hujuma dhidi ya nchi yetu kwa kujua au kutokujua maana kama nchi ikihujumiwa ni wote tunahujumiwa haswa vizazi vijavyo .

Na kama unafanya hivyo kwa makusudi kabisa ujue hautaendelea kuhujumu hivyo maisha yako yote , utashugulikiwa .

Tutangulize maslahi ya nchi mbele .


--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.

Share this :

Related Posts

Previous
Next Post »
0 Comments