[wanabidii] Tamko la wizara ya mambo ya nje juu ya balozi wa china kushiriki shughuli za Siasa ndani ya Tanzania

Wednesday, September 18, 2013
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI


Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa imefuatilia taarifa kwenye vyombo vya habari mbalimbali hapa nchini, kuhusu kushiriki kwa Mheshimiwa Lu Younqing Balozi wa Jamhuri ya Watu wa China hapa nchini kwenye mkutano wa hadhara ulioandaliwa na Chama Cha Mapinduzi (CCM) uliofanyika huko Shinyanga, mwishoni mwa juma lililopita.

Taarifa hizo zimeambatana na picha zinazomuonyesha Mheshimiwa Lu akiwa amevaa kofia yenye nembo ya CCM. Habari zinaeleza kuwa Balozi alikwenda Shinyanga kuhudhuria uzinduzi wa mradi wa viwanda vya kuchambulia pamba vinavyojengwa na mwekezaji wa Kichina anayeitwa Tahong, na viwanda hivyo vita kuwa na uwezo wa kuchambua tani 120,000 za pamba kwa mwaka, vitakapokamilika mwakani.


Wizara inatambua mahusiano mazuri yaliyopo kati ya Jamhuri ya watu wa China na Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na vilevile inatambua kazi nzuri ambayo Balozi Lu Younqing amekuwa akifanya toka alipowasili nchini Tanzania. Kutokana na tukio hili, Wizara inapenda kuelekeza kwamba kitendo cha Balozi yeyote kuhudhuria mikutano ya hadhara ya vyama vya siasa na kuvaa sare zenye nembo ya vyama vya siasa sio sahihi na kinakiuka Kifungu cha 41(1) cha Mkataba wa Vienna wa mwaka 1961, unaoongoza uhusiano wa kidiplomasia. Mkataba huo wa Vienna unazuia wawakilishi wa nchi za nje kujihusisha na masuala ya ndani ya nchi ikiwemo siasa wanapofanya kazi zao kwenye nchi za uwakilishi. Aidha, Sheria ya Diplomasia ya Tanzania ya Mwaka 1986 ambayo ni zao la Mkataba wa Vienna pia hairuhusu Balozi au mfanyakazi wa Ubalozi kujihusisha na masuala ya ndani ya nchi.


Itakumbukwa kwamba, katika kipindi cha mwaka 2010 hadi 2012 Wizara ilikumbana na vitendo vinavyofanana na kitendo hiki na ikachukua hatua stahiki. Na kwa tukio hili pia Wizara imechukua hatua za kidiplomasia zinazostahili ili kuzuia jambo hili lisitokee tena.


IMETOLEWA NA:
WIZARA YA MAMBO YA NJE NA USHIRIKIANO WA KIMATAIFA
18 Septemba, 2013
Dar Es Salaam.

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.

Share this :

Related Posts

Previous
Next Post »
0 Comments