[wanabidii] WASHINDWA KULIPUA BOMU DARAJANI ZANZIBAR

Tuesday, September 24, 2013
Watu wasiofahamika bado, usiku wa kuamkia jana Jumatatu walitupa kitu kinachosadikiwa kuwa bomu lililokuwa katika mfano wa 'sausage' karibu na eneo la biashara kando ya Barabara ya Darajani mjini Zanzibar.

Msaidizi wa Kamishna wa Polisi wa Mkoa wa Mjini Magharibi Zanzibar Mkadam Khamis Mkadam akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake jana kuhusu taarifa hiyo alisema, mlinzi binafsi, Amour Kassim Amour (36), aliyekuwa kazini kwenye
 Duka la Sahara, aliona idadi ya watu katika gari aina ya 'pickup' wakitokea Bwawani kuelekea Mkunazini, walikwenda uelekeo wa dukani alipokuwa akilinda, na walipofika hapo walipunguza mwendo, ndipo mmoja wao aliporusha guruneti upande wake, na kitu hicho kilitua katikati ya masanduku yaliyokuwa mbele ya duka hilo. 

"...lilikuwa likitoa moshi. Kwa ushujaa, Amour aliliokota na kulitupa mbali na maduka," "Kwa bahati, Amour alilitupa kwenye uwanja wa wazi na hakukuwa na wanunuzi katika mtaa huo wenye shughuli nyingi kwa sababu ilikuwa ni usiku," alisema Mkadam akiongeza kwamba guruneti lililipuka kwa mlipuko wenye sauti kubwa dakika chache baadaye. 

Polisi walifanikiwa kupata mabaki ya unga unga na kukusanya kokoto zilizotokana na athari ya mlipuko huo.

Polisi wameanzisha msako na uchunguzi katika tukio hilo, na kuwataka Wazanzibari kuwa watulivu na kuripoti kitu chochote kinachoshukiwa. 


Source: http://www.wavuti.com/4/post/2013/09/wafeli-kulipua-bomu-darajani-zanzibar.html#ixzz2fnWMoop3

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.

Share this :

Related Posts

0 Comments