[wanabidii] MTAA WETU WATEKWA NA MAJAMBAZI

Wednesday, September 25, 2013
Ndugu zangu ,

Jana usiku kuanzia saa 3 usiku ilikuwa mshike mshike mtaani kwetu baada ya majambazi wenye silaha za moto kufanikiwa kuteka mtaa mzima ambapo kuna kituo kikuu kidogo cha mabasi .

Ilikuwa kama sinema vile pale vijana karibu 10 waliposhuka kwenye gari yao na wengine kuanza kurusha risasi hewani na wengine kuanza kwenda sehemu za karibu haswa eneo lenye baada maarufu na maduka maduka na kufanikiwa kutekeleza hiyo hujuma yao ndani ya muda mfupi .

Watu karibu wote walikimbia na eneo hilo liko mbali kidogo na kituo kidogo cha polisi na polisi wenyewe pale pia ni wachache isingikuwa rahisi kupambana na watu hawa kwa jinsi ilivyokuwa inaonekana .

Taarifa hizi ziwafikie costantino kudoja , eng Samson babala na Victor Mwita ambao ni wanachama humu na majirani zangu .

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.

Share this :

Related Posts

0 Comments