[wanabidii] Diwani wa Kiwira ( CHADEMA ) akamatwa kwa kulala na Mwanafunzi

Sunday, September 15, 2013
MNAMO TAREHE 12.09.2013 MAJIRA YA  SAA 19:30HRS HUKO KATIKA KITONGOJI CHA KIBUMBE  KATA YA  KIWIRA – TUKUYU WILAYA YA  RUNGWE MKOA WA MBEYA, RAPHAEL S/O FRANK MIAKA 42, KYUSA, MKULIMA NA MKE WAKESUZANA W/O FRANK, MIAKA 38, KYUSA, MKULIMA WOTE WAKAZI WA KIBUMBE, KIWIRA – TUKUYU  WAKIWA NYUMBANI KWAO WALIGUNDUA KUTOWEKA KATIKA MAZINGIRA YA  KUTATANISHA KWA 
MTOTO WAO AGNES D/O RAPHAEL, MIAKA 18, KYUSA, MWANAFUNZI KIDATO CHA NNE SHULE YA  SEKONDARI KIWIRA HIVYO JITIHADA ZA KUMTAFUTA ZILIANZA MARA MOJA  USIKU KUCHA BILA MAFANIKIO.

MNAMO TAREHE 13.09.2013 MAJIRA YA  SAA 06:00HRS WAZAZI HAO BAADA YA  KUONA MTOTO WAO HAKULALA NDANI KAMA ILIVYO KAWAIDA WALIAMUA KWENDA KATIKA KITUO CHA POLISI KIWIRA NA KUTOA TAARIFA YA  KUPOTELEWA NA MTOTO. HATA HIVYO MAJIRA YA  SAA 09:00HRS MTOTO WAOAGNES D/O RAPHAEL ALIRUDI NYUMBANI NA WAZAZI WAKE WALIPOMHOJI JUU YA  MAHALI ALIPOKUWA ALIWAJIBU KUWA   ALIKUWA NA MHE DIWANI WA KATA YA  KIWIRA [CHADEMA] LAURENT S/O MWAKALIBULE, MIAKA 28, KYUSA, MKAZI WA KIWIRA – KATI NA KWAMBA WALILALA KATIKA NYUMBA YA  MDOGO WAKE NA DIWANI HUYO AMBAYE JINA LAKE BADO KUFAHAMIKA NA KUWA KABLA YA  KUKUTANA WALIWASILIANA KWA NJIA YA  SIMU YA  KIGANJANI.

MTUHUMIWA AMEKAMATWA, UPELELEZI WA SHAURI HILI UNAENDELEA .

KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI DIWANI ATHUMANI  ANATOA WITO KWA JAMII HASA WANAFUNZI KUJIEPUSHA NA MADHARA YA  KUFANYA MAPENZI [NGONO] KWANI NI HATARI KWA  AFYA ZAO NA PIA KWA MAISHA YAO YA  BAADAE BADALA YAKE WAZINGATIE ZAIDI MASOMO KWA FAIDA YAO , VIZAZIVYAO NA TAIFA KWA UJUMLA.
  
[DIWANI ATHUMANI - ACP]
                                                    
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.

Share this :

Related Posts

0 Comments