[Mabadiliko] Abdul Haji shujaa wa westgate mall terror attack

Monday, September 30, 2013
Wanabidii
Nilisikiliza mahojiano ya NTV na ndugu abdul haji aliyejitokeza katika picha nyingi kwenye mkasa wa westgate akijaribu kupambana na magaidi na kusaidia kuokoa watu waliokuwa katika hatari.
Kilichonivutia ni kwamba ndugu huyu wala siyo askari na wala hakuwahi kupitia mafunzo rasmi ya kijeshi. 
Wakati jeshi la kenya na idara nyingine za usalama zikiendelea na maandalizi ndugu huyu alikuwa ndani akipigania maisha ya ndugu zake bila kujari hatari iliyokuwa ikimkabili. 
Aliweza kufanya kwa kiasi alichoweza na kuokoa aliyoweza , alifanya kile ambacho wale wanaoitwa professionals hawakuweza. Hii inatupa somo kwamba huenda vyombo vya usalama havifanyi kazi inayowapasa kufanya au siyo professional kama tulivyoelezwa. Kuna haja si kenya tu hata hapa kwetu kutathmini hali ya idara zetu za usalama kama kweli zinafanya kazi wanazotegemewa kufanya na kama wanao uwezo wa kupambana na matukio kama la west gate.
Pale watu wamekufa, mali imeharibiwa vibaya na gharama kubwa zimetumika lakini magaidi wametokomea wakiwa salama.
Daud

--
Unapokea Email hizi kwa sababu umejiunga na Jukwaa la 'Mabadiliko'.
Kuchangia mada tuma kwenye Email hii: mabadilikotanzania@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda; mabadilikotanzania+unsubscribe@googlegroups.com
Utapokea Email ya kudhibitisha kujiondoa kwako.
 
TEMBELEA Facebook yetu:
http://www.facebook.com/MabadilikoForums?ref=hl
 
For more options, visit this group at:
http://groups.google.com/group/mabadilikotanzania?hl=en?hl=en
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Mabadiliko Forum" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to mabadilikotanzania+unsubscribe@googlegroups.com.
To post to this group, send email to mabadilikotanzania@googlegroups.com.
Visit this group at http://groups.google.com/group/mabadilikotanzania.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.

Share this :

Related Posts

0 Comments