[wanabidii] MTANDAO WA AIRTEL UMETUANGUSHA LEO

Thursday, August 01, 2013
Ndugu zangu

Kwa wale watumiaji wa mtandao wa Airtel wameaona usumbugu mkubwa wanaoupata wanapotaka kuongeza salio kwa njia ya vocha , kuulizia salio na hata kufanya baadhi ya mambo ya mawasiliano kutumia laini hizo za airtel .

Tatizo hili limekaa zaidi ya masaa 24 toka jana mchana lilipoanza mpaka sasa hivi , mimi mwenyewe ndio saa hii Napata sms ya kuniomba radhi lakini hawajasema watafidia vipi hasara nilizoingia kutokana na usumbufu nilioupata kwa masaa 24 sasa .

Nadhani ifike mahali sasa kampuni za simu ziwe zinalipa fidia kwa wateja wao wanapopata usumbufu kama huu na tume ya mawasiliano nayo itoe elimu zaidi kwa watumiaji wa mitandao hii na hata kutoa adhabu kali kwa kampuni za mawasiliano .

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.
 
 

Share this :

Previous
Next Post »
0 Comments