Mialiko ya futari inapogeuka kuwa ya kijamii badala ya kidini.
Na A K Simai
Katika kuperuzi katika mitandao mingi nimebahatika kuona jinsi watu binafsi, makampuni, viongozi wa serikali na watu wengine wakijitahidi katika kuandaa futari na kuwalisha walioalikwa.
Hili ni jambo zuri sana katika mwezi wetu huu mtukufu wa Ramadhaan ambapo tumehimizwa pia zaidi ya kufunga sisi wenyewe pia kukithirisha kufany aibada nyengine ikiwemo kuwalisha na wengine na kufanya hivyo kuna fadhila kubwa ndani yake.- endapo tu kutafanywa kwa ajili ya kupata radhi zake Allaah Subhaanahu Wata'ala na si vyenginevyo. Allaah Subhaanahu anatukumbusha katika Qur'aan Suuratul Insaan 8-12
Na huwalisha chakula, juu ya kukipenda kwake, masikini, na yatima, na wafungwa
Hakika sisi tunakulisheni kwa wajihi wa Allaah. Hatutaki kwenu malipo wala shukrani
Hakika sisi tunaiogopa kwa Mola wetu hiyo siku yenye shida na taabu
Basi Allaah atawalinda na shari ya siku hiyo, na atawakutanisha na Allaah wakiwa na raha na furaha
Na atawalipa kwa Bustani za Peponi na maguo ya hariri kwa vile walivyosubiri.
Hivyo ndivyo anavyotukumbusha Subhaana juu ya wenye kulisha kwa ajili tu ya kupata radhi zake.
Hali halisi ya maisha katika visiwa vyetu inajulikana kuwa ni duni na wananchi wengi ni wale wasiokuwa na uwezo na wasiojiweza. Kuna familia hushindwa hata kupata mlo mmoja wa futari ya maana kwa siku kutokana na ugumu wa maisha unaowakabili.
Tukiwa kama ni viongozi, watu binafsi na hata makampuni , hatuoni haja ya kuwaangalia hawa kwa jicho la huruma japo kwa mwezi huu tu wa Ramadhaan?
Mifano ya mialiko ya futari tunayoiona kwenye mitandao haiakisi hali halisi ya maisha ya mtu wa kawaida kuwa kuona waalikwa wengi ni watu ambao wanaojiweza na kuwepo pale ni kwa sababu tu ya nafasi na hadhi waliyojaaliwa na Muumba.
Kinachosikitisha zaidi ni kwamba mpaka viongozi wa dini nao huingizwa katika mtihani huu kwa kuelewa au kutoelewa kwamba kuwepo kwao katika sherehe za futari za aina hii ambazo zimekuwa za kijamii zaidi kuliko kidini maana yake ni kuzipigia muhuri kwamba hazina tatizo lolote.
Viongozi wetu ndani ya mwezi huu tunawahitajia katika misikiti wakidarsisha, wakisalisha, wakiwaongoza waislamu katika mwezi mtukufu huku wao wenyewe wakiwa mstari wa mbele katika kuzirudisha imani za waumini na dini yao. Kuwaona katika mialiko ya futari ambayo haijalishi kama ni kwa ajili ya Allaah au vyenginevyo kunaweza kupeleka ujumbe mwengine kwa jamii.
Tuna dhamana kama ni viongozi kuhakikisha hatujengi misingi ambayo tutakuja kuwa mas-uul mbele ya Allaah Subhaanahu Wata'ala na pia kuwanasihi viongozi wengine kwa yale yaliyo na kheri na muwafaka kufanywa na waislamu pamoja na wasiokuwa waislamu wanaotaka kulisha katika mfungo wa Ramadhaan kwamba kuzifanya shughuli hizi kwa malengo yale yale yaliyokusudiwa na si kuyageuza kwa malengo mengine.
Viongozi wajenge moyo wa kuweza kufanya maamuzi magumu ya kuzisamehe aina ya shughuli ambazo zitaweza kuwaweka katika mtihani mbele ya Allaah licha ya kuwa karibu na watu. Suuratul Ahzaab /37
Nawe ukawachelea watu, hali Allaah ndiye mwenye haki zaidi kumchelea
Hizi ni nasiha tu kama tulivyoamrishwa na Mtume rehma na amani zimshukie kwamba dini yetu inajengwa na msingi wa nasiha. Ninaamini zitaweza kuwazindua na kuwafaa wale watakaokumbuka kama walikuwa wameghafilika.
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.
0 Comments