[wanabidii] KUMWAGIWA TINDIKALI KWA WAGENI TUJARIBU KUANGALIA UPANDE WA PILI PIA

Saturday, August 10, 2013

Inasikitisha na kuhuzunisha kwa sababu sio mila na desturi ya uungwana wa watu wa Zanzibar lakini ndio ukweli imetokea. Mengi yamesemwa na kuandikwa na kwa ujumla yanaelekea kwa kutuhumiwa kwa Waislam wenye msimamo mkali

Tuviachie vyombo vya sheria vifanye uchunguzi wake lakini kwa mujibu wa maelezo yaliotolewa sio kweli kuwa kuna uwezekano wa muelekeo wa msimamo wa kidini hususan kwa wakati wa tukio lilipotokea maana wengi wa waislam huwa wanafutari kwa wakati huo

Sasa tujaribu kuangalia upande wa pili wa hili tukio Maadui wa Zanzibar na wasiopendelea mafanikio ya nchi hii kuendelea na kujitegemea ikiwemo hawa CCM na Mfumo Kristo inawezekana ndio wanaohusika na tukio hili ili dhamira yao kuifanya Zanzibar ionekane sio nchi ya kutembelewa na watalii ili kudhofisha uchumi na tuendelee kuwa tegemezi la Mkoloni Tanganyika nakuendeleza dhamira yao ya rasimu ya Katiba kutokuwa na serikali tatu ili Zanzibar ionekane kuwa ikiwa itjkuwa na serikali yake machafuko ya kidini yatatakuwapo

Hawa Tanganyika wanajifanya wajanja sana kumbe ni maadui zetu. Sasa ni wakjati wetu Wazanzibari kuamka wana njia nyingi za kutuhujumu nahisi hii ya kumwagiwa tindi kali wageni ni mmoja kati ya hujuma zao Kila tukitaka kuendelea kwa mfano tulikuwa na mpango wa bandari huru wameiuwa na sasa wanajenga kwao Bagamoyo tukitaka kusaidiwa na ndugu zetu Waarabu hutwambia watarudu kututawala halafu huwavamia wao wakaomba misaada na kujengewa kwao huku sisi hatuna tunalolipata na mifano mingi tu

Sasa tujaribu kuangalia pande zote tusiwe tunaangali upande mmoja tu na si hasha mkasikia Sheikh Ponda anahusishwa kwa hotuba au mawaidha yake
Wasalaam

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.

Share this :

Related Posts

0 Comments