Mbunge wa Nzega Hamis Kigwangalla amesema hawezi kumpa kura yake Waziri Mkuu wa zamani na Mbunge wa Monduli Mheshimiwa Edward Lowassa endapo jina lake litajitokeza kama mmoja ya wagombea urais.
Kigwangalla aliyasema hayo wakati akijibu swali aliloulizwa na Fina Mango katika kipindi cha Makutano kuhusu vuguvugu la urais 2015 linaloendelea ndani ya CCM juu ya mgombea urais huku Mheshimiwa Lowassa akiwa kati ya wale wanaotajwa sana kama wagombea hasa katika mitandao ya kijamii.
"Sitompa kura Mheshimiwa Edward Lowassa kwa sababu za msingi tu, kwamba ninakipenda chama changu na nina hakika chama changu kikija na mgombea kwenye uchaguzi mkuu 2015 ambaye ana historia ya

kuhusishwa na mambo machafu kama yale ya Richmond, Dowans ambayo unayasema wewe mwenye hapa tunaweza kupata tabu sana kuomba kura kwa wananchi, lakini pia tutakuwa tumewapa hoja wapinzani wetu ya kusema kwamba tunalea ufisadi, tunaubembeleza ufisadi kwa mikono miwili" Alisema Mheshimiwa Kigwangalla huku akiongezea kuwa Tanzania aihitaji rais asiyeweza kusimamia ukweli.
Akijibu swali kuhusu mitambo ya dowans, Kigwangalla alisema haoni tatizo la mitambo hiyo isipokuwa uamuzi uliotumika katika upatikanaji wake. Katika mahojiano hayo Mheshimiwa Kigwangalla alitangaza nia yake ya kugombea urais mwaka 2025 na kuongezea kuwa 2015 anaona bado ni mapema kwake kwani anaamini watanzania bado hawajamjua Hamis Kigwangalla ni mtu wa aina gani.

Source: http://www.wavuti.com/4/post/2013/08/sitampa-kura-yangu-edward-lowassa-dk-hamis-kigwangalla.html#ixzz2b5ebBjJJ
--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.
0 Comments