[wanabidii] Vuka mipaka wekeza , nchi itakuwa nyuma yako

Monday, July 15, 2013

Mimi ni mmoja wa watu wanaopenda kutafuta fursa za kuwekeza sehemu mbalimbali kwa njia ya mtandao bila ya mimi kunyanyua mguu kwenda huko au hata bila kuwasiliana au kuhitaji msaada wao .

Nikiangalia upande wa watanzania wenzangu haswa vijana naona kama sio watu wanaopenda kupanua mawazo yao na sio watu wa kutafuta fursa mbalimbali haswa zinazohusu mitandao ya kijamii ambayo inaingiza fedha nyingi tu kwa watu mbalimbali sehemu nyingi duniani .

Ukifungua mitandao mingi ya kijamii haswa blogu ,tovuti za habari , kurasa za facebook , majukwaa mbalimbali utashangaa kwamba habari nyingi zinafanana , picha nyingi zinafanana na wachangiaji wengi ni wale wale na mambo mengi pia ni yale yale hii ni ilama ya watu waliokata tamaa wasiopenda kutafuta fursa zaidi hata pale zinapokwisha nchini mwao .

Hii ni rai yangu jioni ya leo kwa Tanzania wenzangu haswa vijana wale waliosoma au wanaopenda masuala ya Tehama , sasa waamke watafute fursa nje ya mipaka ya Tanzania haswa nchi jirani kama Zambia , Malawi , congo drc , Uganda , Kenya , msumbiji .

Nchi hizi au tuseme maeneo haya yanafursa nyingi sana zinazohusiana na TEHAMA haswa kwa njia ya mtandao na ndugu zangu watanzania tukijipanga vizuri tunaweza kuingia kwenye masoko hayo ya kuleta faida kwa maisha yetu na nchi yetu .

Hii mitandao ya nchi jirani tukiweza kuishika vizuri na kuwa na mashabiki wengi wanaotufuatilia hata pale nchi yetu inapokuwa na tishio toka kwenye nchi hizo ni mitandao hii hii inayoweza kutumika kwa maslahi yetu , hata pale jina la nchi linapochafuliwa ni mitandao hii hii inayoweza kutumika kuisafisha na kuendelea mbele zaidi .

Tumeona baadhi ya wananchi wa nchi jirani wanavyotumia udhaifu ulioko kwenye vyombo vyetu vya mawasiliano haswa mitandao ya kijamii kujipenyeza kwenye biashara , ujasusi , propaganda na mambo mengine mengi tu kwa maslahi yao sasa hii isiachwe iendelee hivi hivi .

Vuka mipaka wekeza , nchi itakuwa nyuma yako .


--
Find Jobs in Africa Jobs in Africa
International Job Opportunities International Job Opportunities
Jobs in Kenya Jobs in Kenya

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.
 
 

Share this :

Related Posts

0 Comments