Ndg wanabidii
nimesikiliza Radio BBc na imehabarishwa kuwa zaidi ya watu laki moja wameuwawa na maelfu kujeruhiwa nchini Misri. Kisa ni mapambano kati ya Polisi na wafuasi wa Rais aliyepinduliwa Bw. Morsi.
Kwa hali hii mtu yeyote anayejali UTU na kuheshimu kuwa UHAI ni zawadi ya kwanza na kubwa, Mungu aliyejaliwa viumbe wake inaumiza. Sidhani kama maisha yawe ya mwanadamu au kiumbe chochote yamekosa thamani kiasi hiki. Ni lazima dunia ielimishwe THAMANI ya uhai wa MTU. Na UHAI utunzwe na uheshimike. Madaraka na nguvu ni BAADA ya Uhai na si KABLA ya Uhai.
Kama ni darasa limetoshwa na naomba lieleweke kwa Watanzania. Unapoua unapigania nini?
nawakilisha.
0 Comments