[Mabadiliko] Obama Hafichi Kusimulia Alikotoka, Anasema; " Nilidunduliza nikanunua suti na viatu vilivyonibana!"

Sunday, June 30, 2013

Obama Hafichi Kusimulia Alikotoka, Anasema; " Nilidunduliza nikaweza kununua suti na viatu vilivyonibana, ofisini walishangaa!"

Ndugu zangu,

Obama anasema; " Wakati tukiendelea na masomo yetu ya Sheria mimi na Michelle tulifanya kazi katika kampuni ya Uwakili ya Sidley na Austin jijini Chicago.

Binafsi nilikuwa na wasi wasi kuhusu ujana wangu na hasa changamoto kuwa maisha ya sasa ni fedha. Hofu yangu ilikuwa ni lini nitaanza kukamata fedha nyingi ili zisaidie mawazo na fikra zangu kufikia mahala ninapotaka.

Lakini, kutokana na kupanda kwa gharama na mkopo niliyochukua Serikalini kwa ajili ya masomo, niliamua kuendelea kuwatumikia mabwana wawili; chuo na kampuni ya sheria.

Nilijitahidi kadiri nilivyoweza kundunduliza sehemu ya kipato changu . Hatimaye nilifanikiwa kuwa na chumba. Nilinunua suti zangu tatu na pia jozi moja ya viatu.

Hata hivyo, wakati nanunua viatu sikuwa makini, kwani vilionekana vidogo; vilivyonibana na kunifanya nionekane mshamba. Siku niliyopiga ripoti ofisini, kila mmoja aliniangalia.

Ingawa sikujua ni kwa nini, lakini nilihisi walifanya hivyo kutokana na viatu vyangu!"- Barack Obama ( Kutoka kijitabu cha Maisha Ya Barack Obama, alikotoka, aliko na anakokwenda, Maggid Mjengwa, 2008.)

Maggid,
Iringa.
0754 678 252
http://mjengwablog.com

--
Unapokea Email hizi kwa sababu umejiunga na Jukwaa la 'Mabadiliko'.
Kuchangia mada tuma kwenye Email hii: mabadilikotanzania@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda; mabadilikotanzania+unsubscribe@googlegroups.com
Utapokea Email ya kudhibitisha kujiondoa kwako.
 
TEMBELEA Facebook yetu:
http://www.facebook.com/MabadilikoForums?ref=hl
 
For more options, visit this group at:
http://groups.google.com/group/mabadilikotanzania?hl=en?hl=en
 
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Mabadiliko Forums" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to mabadilikotanzania+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.
 
 

Share this :

Previous
Next Post »
0 Comments