[wanabidii] Dk Slaa:Tuhuma za Lwakatale, kuteka waandishi zimepikwa

Thursday, March 14, 2013
WAKATI Jeshi la Polisi nchini ikiendelea kumshikiria Mkurugenzi wa
Usalama na Ulinzi wa Chadema Willifred Lwakatale kwa mahojiano zaidi
kwa siku ya pili, Katibu Mkuu wa chama hicho Dk Willibroad Slaa
amesema tuhuma hizo ni za kupikwa.

Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam,Dk Slaa
alisema kwamba tuhuma zinazomkabili Lwakatale ni za uongo na
zimepikwa, hivyo wanaitaka jeshila la polisi kuendelea na uchunguzi wa
suala hilo na wakikamilisha kazi yao wampeleke Mahakamani.

"Hizo tuhuma ni za uzushi, hazina ukweli hata kidogo, zimepikwa hivyo
tunaiomba Jeshi la Polisi kuendelea na kazi yao na mwisho wamfikishe
Mahakamani kwa sababu huko ndipo tutakapo pata ukweli juu ya suala
hilo"alisema Dk Slaa.

Mkurugenzi huyo alikamatwa na Polisi jana kwa tuhuma za kuhusika
katika njama za kumteka na kumtesa Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri
(TEF) na Mhariri Mtendaji wa Kampuni ya New Habari Absalom Kibanda.

Mbali na tuhuma za kumteka Kibanda,pia anahojiwa kwa tuhuma ya kushiki
njama mbalimbali za mauaji pamoja na mateso ya Mussa Tesha
aliyemwagiwa tindikali Igunga na lile la morogoro ambapo kijana mmoja
alifariki katika vurugu za maandamano ya chadema, ambapo polisi
walitoa taarifa kuwa kijana huyo ameangukiwa na kitu kizito. Pamoaja
na kuandaa njama za kumteka Mhariri Mtendaji wa Gazeti la Mwananchi
Denis Msacky ambazo bado hazijatekelezwa.

--
Jobs in Africa - www.wejobs.blogspot.com
International Jobs - www.jobsunited.blogspot.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.

Share this :

Related Posts

0 Comments