[wanabidii] ULEAJI WA VIFARANGA VYA KUKU SIKU 1 HADI WIKI 5

Tuesday, February 05, 2013
Kwa kawaida au katika hali halisi, kazi ya kulea vifaranga hufanywa na
kuku mwenyewe. Hivyo ili kulea vifaranga, mfugaji ni lazima aige kuku
anavyofanya. Ikumbukwe kuwa vifaranga husumbuliwa zaidi na hali
mbaya ya hewa, magonjwa mbalimbali, kukosa chakula kisichofaa na
kukosa uangalizi wa karibu.
Ni lazima vifaranga waangaliwe kwa kuwapatia nyumba yenye joto,
chakula kinachofaa na maji safi, kuwakinga dhidi ya magonjwa
masumbufu kwenye eneo husika na kuwatibu wanapougua. Mfugaji
anayefanikiwa ni yule anayelea vifaranga wenye afya nzuri ambao
hatimaye hutoa mazao mengi yanayompa faida.
Wafugaji wengi vijijini wamezoea kumwachia mama kuku kufuga vifaranga
wake kwa muda mrefu hadi wajitegemee. Njia hii humchelewesha kuku
kurudia kutaga na hivyo kupata vifaranga wachache zaidi kwa mwaka.
Lakini vifaranga vikiondolewa kwa kuku mapema, kama majuma matano
hivi baada ya kuanguliwa, na wakatunzwa na mfugaji, kuku hutaga
mapema na idadi ya kuku kwa mfugaji huongezeka haraka ndani ya
kipindi kifupi. Jifunze namna ya ufugaji bora wa vifaranga hapa
http://achengula.blogspot.com/


--


*To all the questions of your life YOU are the most possible answer. To
all the problems of your life YOU are the best solution. Trust yourself*

--
Jobs in Africa - www.wejobs.blogspot.com
International Jobs - www.jobsunited.blogspot.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.

Share this :

Related Posts

0 Comments