[wanabidii] TAMKO LA CCM KUHUSU MAANDAMANO NA VURUGU ZILIZOTOKEA JUU YA UJENZI WA BOMBA LA GESI NA MAENDELEO YA MKOA WA MTWARA

Wednesday, February 13, 2013

TAMKO LA HALMASHAURI KUU YA TAIFA YA CCM KUHUSU MAANDAMANO NA VURUGU ZILIZOTOKEA MKOANI MTWARA JUU YA UJENZI WA BOMBA LA GESI NA MAENDELEO YA MKOA WA MTWARA


1. Halmashauri Kuu ya Taifa imepokea maelezo ya Serikali kuhusu maandamano na vurugu zilizotokea Mkoani Mtwara tarehe 27 Desemba, 2012 tarehe 25 Januari, 2013 na tarehe 26 Januari, 2013. Maandamano na vurugu hizo zilizodaiwa kuwa na lengo la kupinga mradi wa bomba la Gesi kujengwa na kupeleka Gesi Dar es Salaam.

2. Baada ya kupokea maelezo haya ya Serikali, Halmashauri Kuu ya Taifa imebaini kuwa: -

(a) Kwa sehemu kubwa Wananchi wa Mkoa wa Mtwara hawakuwa wamepewa elimu ya kutosha juu ya uendelezaji wa Gesi na jinsi watakavyonufaika.

(b) Baadhi ya Wanasiasa na baadhi ya Viongozi wa Makundi mbalimbaliwaliamua kutomia suala la Gesi kupandikiza lugha za chuki, uchochezi na upotoshaji wa maendeleo ya Mradi wa Gesi kwa lengo la kujitafutia umaarufu.

(c) Suala la Gesi limetumika kama kisingizio tu cha kufanya vitendo vya rurugu na uvunjifu wa amani.

3. Kutokana na ukweli huu, Halmashauri Kuu ya Taifa inaelekeza ifuatavyo:-

(i) Imesikitishwa na vurugu zilizotokea na kusababisha watu kadhaa kupoteza maisha na uharibifu mkubwa wa mali na majengo ya CCM,Serikali, Wabunge na watu binafsi. Halmashauri Kuu ya Taifa inawapa pole wafiwa na waliopoteza mali zao.

(ii) Inaiagiza Serikali kufanya uchunguzi wa kina kuhusu waliofanya vurugu na uharibifu mbalimbali na kuwachukulia hatua kwa mujibu wa Sheria. Pia, kuwa makini na kuhakikisha matukio kama haya hayajitokezi tena.

(iii) Inaiagiza Serikali kuendelea kutoa elimu ya kutosha kwa Wananchi wamaeneo husika kuhusishwa na kuelimishwa juu ya miradi mbalimbali kwenye maeneo yao.

(iv) Halmashauri Kuu ya Taifa inawataka Wananchi wa Mkoa wa Mtwara kuendelea kuishi kwa amani na utulivu kama ilivyo desturi yao, maana vurugu pamoja na kuharibu mali na kugharimu maisha vinaweza kuwakimbiza wawekezaji waliojitokeza na ambao shughuli zao zitawafaidisha wananchi wa Mkoa huu na Watanzania kwa ujumla .

HALMASHAURI KUU YA TAIFA
Dodoma 10 – 11 Februari, 2013


Source: http://www.wavuti.com/#ixzz2KnmKVHrY

--
Jobs in Africa - www.wejobs.blogspot.com
International Jobs - www.jobsunited.blogspot.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.
 
 

Share this :

Related Posts

0 Comments