Chadema to pay heavy fine or be out of politics for a time or both!
Lile blog linalojulikana kwa jina la kipiganaji (nom de guerre) kama'THE MOUTH OF THE SOUTH' – likipata jina hilo baada ya kusimama imara pamoja na watu wa Mtwara katika ile kesi ya gesi ambayo bado haijesha – yaani lile blog la Zanzibar Ni Kwetu (ZNK), inasemekana watendaji wake leo walikuwa mbioni kwa miguu na kwa magari wakienda huku na kule hapa Zanzibar Mjini na huku wakiwa out of mood completely kuzungumza na mtu yoyote yule. Hali hio imejitokeza baada ya ile tamaa yao ya kuiona Chadema inachukua nchi 2015 sasa ikawa haipo. Sababu kubwa ni kule Chadema kutoa nambari binafsi ya simu ya Spika na Kaimu Spika kwa wananchi - nambari ambazo hata kwenye website ya BUNGE hazimo. Jambo hili limeleta taabu kubwa sana kwa Spika na kwa Kaimu Spika, kwani wamepokea SMS tele tu zikiwatukana mpaka matusi ya nguoni na ushahidi wanao bado kwenye simu zao. Inasemekana mpaka wakati huu Spika ameshapokea zaidi ya SMS 500 na simu 300 za matusi, kejeli na maneno mengine ya ovyo.
"Kama wakienda mahkamani huyu Spika Anna na huyu Kaimu Spika Ndugai ni kuwa Jaji atakubali kama ninavyokubali mimi na wewe kuwa hili nikosa kubwa sana, tena la jinai", aliendelea kinara wa ZNK," Na kama Jaji atatoa hukumu ya haki bila ya upendeleo, basi Chadema itaweza kufungwa kwa muda fulani au itabidi ilipe mamilioni ya pesa, au yote mawili", aliendelea huyo kinara wa ZNK huku akisikitika kama vile kapoteza jamaa yake kwa kifo cha ghafla.
"Kama ulivyosoma juu ya mapendekezo ya Chadema kwa Katiba Mpya, sisi tamaa yetu kubwa ya kupata Jamhuri yetu ya Watu wa Zanzibar ipo mikononi mwao (Chadema), kwani tunajua kuwa wao wakipata tu basi wataikata kamba na tutakuwa huru kama tulivyokuwa tarehe 25 April, 1964, lakini hivi sasa hatujui kama huyu Spika na Naibu Spika watachukua hatua gani. Vyenginevyo, bila ya Chadema tumekwisha, Zanzibar huru itabakia kuwa nyimbo ya watoto wadogo mitaani tu!
"La kuomba ni kwamba, huyu mama awe kama mama wa kweli – yaani awe mwingi wa huruma na asichukue hatua zozote zile za kisheria dhidi ya Chadema. Kinyume cha hivyo ni kuwa Chadema itakuenda na maji kama lilivyokuenda na maji gazeti la Mwanahalisi, kwasababu haitoweza kulipa fidia ambayo Anna na Ndugai wataidai kupitia mahkama. Pia, hata wakiweza kulipa hio fidia, je, Jaji akitoa hukumu ya Chadema kuenda jela miaka 2 itakuaje? Sote tunafahamu nini maana ya chama kuenda jela na hilo hatuliombi sio kwa Chadema tu bali kwa Mtanzania yoyote yule. With the general elections hardly 2 years away, Chadema cannot afford to lose a single day out of politics", alimalizia kingwengwe huyo wa Zanzibar Ni Kwetu, wakati alipokuwa akizungumza na Wagagagigikoko pale Muembe Rikunda, Zanzibar, baada ya kufuatwa kwa muda wa zaidi ya masaa 2 ili atoe tamko rasmi la Zanzibar Ni Kwetu kuhusu hii kashfa.
0 Comments