TAARIFA KWA UMMA
YAH: MAZUNGUMZO YA WABUNGE WA MKOA WA DAR ES SALAAM NA WAZIRI MKUU, DODOMA -TAREHE 07.02.2013
Waziri Mkuu, Mheshimiwa Mizengo Pinda jana tarehe 7.2.2013 alifanya kikao na Wabunge wa Mkoa wa Dar Es Salaam na kuhudhuriwa na Waheshimiwa Abasi Zuberi Mtemvu ambaye ni Mwenyekiti wa Wabunge wa Dar es Salaam, Iddi Azzan, Mussa Azzan Zungu, Eugen Mwaiposa, Neema Himid, Mariam Kisangi, Phillipa Mturano, Halima Mdee, Dkt Milton Mahanga, Sophia Simba na Dkt Faustine Ndugulile. Kwa upande wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi iliwakilishwa na Waziri Anna Tibaijuka na Naibu wake Goodluck Ole Medeye. Kikao hiki pamoja na mambo mengine, kilijadili suala la Mji Mpya wa Kigamboni.
Katika kikao hiki nilielezea kuwa dhana ya Mji Mpya wa Kigamboni ni nzuri, ila mchakato wa kufikia huko unakabiliwa na changamoto nyingi ikiwa ni pamoja na ukiukwaji wa sheria unaofanywa na viongozi na watendaji wa Wizara ya Ardhi. Nilitabanaisha kuwa sheria kama sheria ni nzuri na hazina matatizo yoyote, ila utekelezaji wa sheria hizi umekuwa na mapungufu makubwa.
Ikumbukwe kuwa mchakato huu unatawaliwa na sheria tano ikiwa ni pamoja na Sheria ya Utwaaji Ardhi na. 47 ya mwaka 1967; Sheria ya Mipango Miji na. 8 ya 2007; Sheria ya Ardhi no. 4 ya 1999; Sheria ya Wakala wa Serikali ya 1997 na Sheria ya Serikali ya Mitaa na.8 ya 1982.
Pili, ushirikishaji hafifu wa wananchi, viongozi wa Serikali na wawakilishi wa wananchi ikiwa ni pamoja na Mbunge wa eneo husika. Waziri na Watendaji wa Wizara wamekuwa hawafuati sheria na badala yake kumekuwa wakitumia ubabe, nguvu na usiri mkubwa katika utendaji kazi wao. Aidha, wananchi wamekuwa wakitaarifiwa na sio kushirikishwa katika mchakato wa mradi huu. Kuna tofauti kubwa kati ya kutaarifu na kushirikisha.
Aidha, kuongeza eneo la mradi toka ekari takribani 6,000 hadi kufikia ekari 50,000 bila kuwashirikisha wananchi wa maeneo ya Kisarawe II, Kimbiji, Pemba Mnazi na Somangila kumeleta taharuki kwa wananchi wengi wa maeneo haya.
Vile vile, uanzishaji wa Mamlaka ya kusimamia uendelezaji wa Kigamboni, Kigamboni Development Authority (KDA), umeleta mtafaruku mkubwa katika Halmashauri ya Manispaa ya Temeke kuhusu mamlaka na mipaka kati ya KDA na Manispaa, mamlaka ipi itenge bajeti ya kuendeshea kata chini ya Mradi huu na hatma ya Madiwani katika eneo la mradi.
Vile vile, kutokana na usiri mkubwa kwenye mradi huu wananchi wengi hawafahamu lengo la mradi, haki, stahili na hatma yao.
Katika kikao hiki nilitoa mapendekezo yafuatayo:
HITIMISHO
Katika kuhitimisha. Waziri Mkuu alipitia mapendekezo na kusisitiza mambo yafuatayo:
Napenda kuwashukuru Wabunge wa Mkoa wa Dar Es Salaam kwa ushirikiano walioonyesha na kwa michango mizuri katika kikao hiki. Kwa aina ya pekee, ninamshukuru Waziri Mkuu, kwa kuendesha vizuri kikao hiki kwa hekima na busara.
Ninawaomba wananchi wa Kigamboni kuendelea kuwa watulivu, wakati mimi na Wabunge wenzangu wa Dar Es Salaam tukiendelea kufuatilia utekelezaji wa maagizo ya Waziri Mkuu na pia majibu ya hoja zilizotolewa. Mwisho, niwatake Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kuendesha mchakato huu kwa mujibu wa sheria, kwa kuzingatia dhana ya utawala bora na kwa taratibu shirikishi.
Dkt Faustine Ndugulile (MB)
JIMBO LA KIGAMBONI
Source: http://www.wavuti.com/#ixzz2KKsI8dC4 --
Jobs in Africa - www.wejobs.blogspot.com
International Jobs - www.jobsunited.blogspot.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.
0 Comments