Marehemu Namsifu alikuwa mjasiria mali mdogo mwendesha pipipiki. Siku ya tukio marehemu alitumwa na mke wa muuaji Baba John waliyetaka kutalakiana ambaye ni mkaazi wa Bubombi kupeleka waraka wa mahakama kwa Baba John kupitia Ofisi ya Serikali. Inasemekana merehemu alifika ofisi ya Serikali ya kijiji Kogaja alikuta viongozi wako
kwenye kikao wakamwambia asubiri. Punde kidogo Baba John alifika na alimteka Marehemu kimazingira na kujikuta kwenye himaya ya muuaji huyu mkatili kuliko wote niliowahi kuwasikia.
Baada ya marehemu kutorudi kamwe makazi yake ya Bubombi ndugu na jamaa pamoja na wakazi wa Bubombi ambako marehemu ni mtu maarufu kutokana na tabia yake ya ucheshi na kuwa mlinda lango wa timu ya kijiji walianza kumtafuta na kituo cha kwanza kikiwa kijiji cha Kogaja alikotumwa marehemu kupeleka Waraka wa mahakama. Walienda hadi nyumbani kwa muuaji wakamkuta anafunguo za pikipiki za marehemu Namsifu hukupikipiki ikiwa karibu na ofisi ya kijiji.
Baada ya mahojiano mtuhumiwa alikiri Namsifu alifika kwake akamwambia amshikie funguo za pikipiki. Baba John alikamatwa na kupelekwa kituo cha polisi. Msako ulifanyika nyumbani kwake na siku ya Ijumaa hii watu waliripoti kupata shati la marehemu Powe nyumbani kwa Baba John. Katika msako zaidi nyumbani kwa mtuhumiwa vimekutwa viungo vya marehemu vimetawanywa na vikaanza kuokotwa moja baada ya kingine. Mikono kwingine, kichwa kimebong'olewa huko, miguu vipande huko. Viungo kuanzia kiunoni, tumboni na vya uzazi vikiwa vimekosekana hadi sasa. Anapoulizwa anasema alivigawa kwa mganga mwenzie Mkenya (mtuhumiwa inasemakana ana asili ya
Kenya japo ni mkaazi wa Kogaja).
Baba John sasa aliyekiri kufanya mauaji hayo ni mganga nguli mwenye wateja maarufu wilayani Rorya ikijumuisha mfanyabiashara mmiliki wa Hoteli maarufu jijini Mwanza, maduka, vyombo vya usafirishaji, Zabuni za Serikali na Mwanasiasa. Ushahidi wa Baba John kwamba gari analotembelea amenunuliwa na Mfanyabiashara huyu.
Huu ni ukatili ambao hauwezi kuvumiliwa na jamii yoyote ya kiistarabu. Tunawataka wateja wa baba John anaowafanyia Uuguzi kwa ushirikina kuacha kuingilia Sheria ichukue mkondo wake na haki itendeke. Polisi walifanya vizuri kuweka ulinzi eneo la tukio kwa mtuhumiwa. Ninasema haya kwa kuwa ni dhahiri nchi hii sasa wenye pesa wanaweza kufanya lolote na Baba John pengine alitegemea watu maarufu wanaoweza kumtetea hata akifanya huu
unyama wa kutisha.Wana Rorya tuwakatae watu kama hawa kwenye jamii zetu. Kitu cha pili tunaharibu sifa ya jamii yetu.
Imeandikwa na:
JACOB NYONGESA SWERE
Source: http://www.wavuti.com/#ixzz2Lw2FgTL2 --
Jobs in Africa - www.wejobs.blogspot.com
International Jobs - www.jobsunited.blogspot.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.
0 Comments