[wanabidii] TANGAZO LA MKUTANO WA HADHARA WA TAMICO UTAKAOFANYIKA GEITA SIKU YA JUMAMOSI TAREHE 05/01/2013.

Thursday, January 03, 2013

Wadau,

Heri ya mwaka mpya na hongereni kwa majukumu ya ujenzi wa Taifa. Kwa Bahati mbaya huku migodini tumeuanza mwaka 2013 kukiwa na uzushi uliozagaa wa kusitishwa kwa fao la kujitoa ifikapo February 2013. Uzushi huu umezagaa karibu migodi yote ya dhahabu na umesababisha wimbi kubwa la wafanyakazi wa migodini kuacha kazi ili wawahi tarehe hiyo ya kizushi.

Cha kushangaza waajiri wako kimya na wanakubali wafanyakazi wao kujiuzuru kwa uzushi huo pasipo kuwaelimisha na kuwapatia taarifa sahihi wafanyakazi  ambao wamewazalishia mali kwa muda mrefu na kwa faida. Ukimya huu wa waajiri unaibua maswali na mashaka na kudhania yawezekana wakawa na mkono katika uzushi huu ili wanufaike na kupunguza wafanyakazi kwa gharama nafuu.

Binafsi kama kiongozi wa TAMICO nalaani wazushi wenye nia mbaya ya kuhujumu haki za wafanyakazi na jitihada za serikali za kuwapatia wananchi wake ajira na maisha bora, badala yake watu wachache wanatumia mwanya wa kupindisha ukweli kwa lengo la maslahi binafsi.

Kama sehemu ya kuelimisha umma, TAMICO imeandaa mkutano wa hadhara utakaofanyika Jumamosi tarehe 05/01/2013. Mkutano huu utafanyika katika viwanja vya kanisa Katoliki mjini Geita kuanzia saa 8:00 mchana na kuendelea. Mkutano huu unatarajiwa kuhudhuriwa na viongozi na wawakilishi wa TAMICO kutoka sehemu mbali mbali za kazi.

Mgeni rasmi atakuwa ni Mheshimiwa Suleiman Jaffo, mbunge wa Kisarawe na mtoa hoja binafsi ya kutaka  sheria ya marekebisho ya sheria za mifuko ya hifadhi ya jamii,2012 (hususani fao la kujitoa) ipitiwe upya. Wanachama wa mifuko ya hifadhi ya jamii na wafanyakazi wote bila kujali itikadi yoyote ile mnaalikwa kuhudhuria bila kukosa ili kupata ufafanuzi wa kina wa hatma ya fao hilo na kipi kinafanyika kwa sasa kuhusiana na sheria hiyo.

Wote mnakaribishwa kuhudhuria na/ au kutoa maoni ambayo yatanusuru wimbi hili linalowanyima wafanyakazi fursa ya kufanya kazi kwa manufaa ya familia zao na taifa kwa ujumla.

Nawasilisha,

 

Thomas Sabai

Katibu wa TAMICO- Tawi la GGM

--
Jobs in Africa - www.wejobs.blogspot.com
International Jobs - www.jobsunited.blogspot.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
 
 

Share this :

Previous
Next Post »
0 Comments