[wanabidii] serikali haijawaelewa watu wa Mtwara

Thursday, January 03, 2013
                         natia wasi wasi na uelewa wa viongozi wetu, sijui niwaite watawala,
wananchi wa Mtwara hawajasema hawataki gesi isitumike kwa watu wengine, au ni lazima watumie wao tu, si kweli
watu wa mtwara wanataka si tu kushirikishwa bali hata kufaidi juu ya gesi hiyo ikiwa pamoja na kufungua viwanda hivyo na wao wakapata ajira, wanaogopa falsafa ya kivuli cha mti wa mvuno ambao kimvuli cha mti huo hutua mbali sana na hivo kimvuli icho hakimfaidishi alie panda mti huo, hivi ina yamkinika MAFINGA-IRINGA pamoja na msitu mkubwa kiasi kile lakini wanafunzi wanakaa chini madarasani na wengine wanaweka viroba vikiwa vimejazwa mchanga ndo wanakalia, baba zao na mama zao waliulinda ule msitu kwa mali na kwa hali zao zote.....rejea film ya Darwin's nightmare(filamu ya mapanki) iliyo onyesha jinsi gani wananchi wa Mwanza walivo na wanavokula mapanki alafu minofu ya samaki inapelekwa nje
watanzania tufunguke tukichekeana nchi itaharibika, hata Somalia na siera lione ilianza hivi hivi

Share this :

Previous
Next Post »
0 Comments