*TAARIFA KWA UMMA*
NAPENDA kutoa taarifa kwa umma kutokana na habari zinazoandikwa kwenye
baadhi ya vyombo vya habari, huku chanzo cha habari hizo kikiwa ni Katibu
wa BAVICHA Mkoa wa Tanga, Bwana Deogratias Kisandu, ambazo zimekuwa
zikionesha kuwa vijana wa Mkoa wa Tanga tuna walakini katika chama chetu
cha CHADEMA.
Leo katika baadhi ya vyombo vya habari, Bwana Kisandu amenukuliwa akitoa
taarifa kuwa yeye pamoja na makatibu wenzake nchi nzima, wamepanga kufanya
maandamano ya kuupinga uongozi wa juu wa kitaifa wa BAVICHA.
Kwa kutambua na kuheshimu kuwa moja ya misingi muhimu ya uendeshaji wa
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) pamoja na mabaraza yake ni
vikao, ambavyo vipo kwa mujibu wa Katiba, miongozo, taratibu, kanuni na
itifaki za chama, vijana wa CHADEMA Mkoa wa Tanga, ambao mimi ndiye msemaji
wao kikatiba, tunaamini Bwana Kisandu anazidi kupotoka.
Kwa hiyo basi, kama ambavyo nimeshapokea malalamiko kutoka kwa vijana wa
Tanga baada ya hatua yake ya awali ya Bwana Kisandu kutoa taarifa kwa
vyombo vya habari, bila kuzingatia katiba, maadili na itifaki ya chama,
akibeba propaganda nyepesi za Sekretarieti ya CCM, juu ya suala la kadi
mbili kwa Katibu Mkuu wetu Dkt. Willibrod Slaa, kuna haja ya kufanya vikao
kuangalia na kujadili mwenendo wa kiongozi mwenzetu huyo.
Kwa sababu kama vijana makini wa CHADEMA, chama ambacho kinaamini katika
kutoa utumishi bora, mikakati madhubuti, sera imara kwa ajili ya maendeleo
endelevu ya Watanzania wote, ambao wamekosa uongozi bora na siasa safi
kutokana na ufisadi na ubadhirifu wa CCM, lazima tuwe makini na kila
mwenzetu yeyote yule ambaye anaonekana kufanya kazi ya CCM kwa kutumia jina
la CHADEMA.
Tunapenda kumkumbusha Bwana Kisandu kuwa atumie muda wake pia kuisoma vyema
katiba ya CHADEMA hasa katika Sura ya 10 inayozungumzia Maadili ya
Viongozi, Sifa mahususi za viongozi na maadili ya wanachama, kifungu
10.1(1-13), toleo la mwaka 2006.
Kuhusu masuala ya ushiriki wa vijana kwenye shughuli mbalimbali za chama
ikiwemo mikutano ya M4C, Bwana Kisandu anapaswa kuelewa kuwa vijana
kutokana maeneo mbalimbali ya nchi, ukiwemo Mkoa wa Tanga tumekuwa
tukishirikishwa, kupitia utaratibu maalum unaopangwa na Ofisi ya Katibu
Mkuu, ambao tunaamini mpaka sasa umetoa fursa kwa wanachama wote, wakiwemo
wazee, wanawake na vijana kukieneza na kukiimarisha chama maeneo mbalimbali
ya nchi.
Na maamuzi yote ya msingi kwa uendeshaji wa Baraza hasa kwa Mkoa wa Tanga
yatafanyika kupitia vikao na hatua zitachukuliwa kwa kufuata katiba,
kanuni, maadili, itifaki na miongozo ya chama.
*Aron J Mashuve*
*Mwenyekiti wa BAVICHA*
*Mkoa Wa Tanga*
--Jobs in Africa - www.wejobs.blogspot.com
nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com
DELL LATITUDE D 620 & D30
80 GB HardDisk ,CORE 2 DUO , 2.0 GHZ CPU ,1 GB RAM
DVD/CD - RW ,WINDOWS 7 /WINDOWS XP ,WIRELESS , BLUE TOOTH .
TSHS : 380,000 , 1 YEAR WARRANTY
CALL : 0786 806028
Free Delivery in Dar es salaam
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
0 Comments