[wanabidii] Mwaka mmoja bila Halima Mchuka

Friday, December 28, 2012

Disemba 29, 2011 Tanzania ilimpoteza mwanahabari mahiri, mpenda
kazi, mwalimu na mwanamke aliyependa maendeleo ya jamii yake
katika michezo nchini Tanzania Bi Halima Mchuka na kuleta upweke
kutokana na msiba wake.

Kilio cha msiba wake kiliwakutanisha wanahabari wote walio katika
vyombo vya umma na binafsi, huku Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania, mpenda michezo Jakaya Kikwete akishiriki kwa karibu
katika msiba wa mwanahabari huyo ambaye mimi binafsi nilipata
nafasi ya kuwa nae karibu huku nikijifunza mengi kutoka kwake.

Leo hii ninapoandika haya ni siku 365 tangu Bi Mchuka afariki
dunia. Ndoto zake nyingi zikiwa hazikukamilika ziwe kwa jamii
yake, familia yake na ata taifa lake la Tanzania.

"Makwega nilikuwa namtafutia sehemu mwanangu afanye mazoezi
hivi sasa anasoma huko Uganda, lakini nilipewa ahadi mpaka sasa
binti yangu hajapata." Alinidokeza Marehemu Halima Mchuka katika
mazungumzo nami mwaka 2011.

Maelezo haya ya dada Halima yanaonyesha kuwa alikuwa mzazi
aliyetaka maendeleo ya masomo kwa watoto wake, kwani elimu ni jambo
la msingi kwa kila kizazi ili kiweze kupambana na mazingira
yanayoizunguka jamii husika.

Pia alitambua kuwa elimu ya darasani haitoshi bali vijana
wanahitaji mno mazoezi ili kuweza kufanya vizuri wanapopewa majukumu
kama ilivyo katika michezo.

"Jamani, sasa hivi unatangaza vizuri tatizo lako la r na l
limekwisha, unajua wakati ule ulikuwa unatangaza kwa upole na
unyonge lakini sasa unachangamka sana katika mike." alisema Dada
Halima Mchuka alilpokuwa akionyesha kuwa alikuwa akifuatilia kwa
karibu namna mtangazaji mpya alivyokuwa akifanya kazi yake na
kujifunza kazini, Hongera dada Halima, Mungu akulaze pema.

Kutambua na kukubali kuwa mwenzako anajifunza na ana maendeleo ni
jambo adimu, lakini Dada Mchuka alikuwa akionyesha na alikuwa
akipongeza na kuwatia moyo sana vijana waliokuwa wakijifunza taaluma
hii ya habari na hasa utangazaji, nikiwamo mimi .

Imekuwa vigumu mno kumsahau kwani mchango wake ni mkubwa katika
michezo si kwa kuwa mwanamke wa kwanza tu kutangaza mpira wa miguu,
bali alikuwa mwanamke mpenda maendeleo ya binadamu mwingine
kitaaluma na kimaisha.

Dada Halima wanao wanalia, rafiki zako wanalia, wanamichezo wanalia,
Simba wanalia, Yanga wanalia, kaka yako Sued Mwinyi analia, Shida
Masamba mdogo wako analia na Kaka yako Chrispine Lugongo analia.

Najua, wewe umetangulia bali safari hii ni safari ya wote.

Wasalaam Adeladius Makwega.

--
Jobs in Africa - www.wejobs.blogspot.com
nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com

DELL LATITUDE D 620 & D30

80 GB HardDisk ,CORE 2 DUO , 2.0 GHZ CPU ,1 GB RAM
DVD/CD - RW ,WINDOWS 7 /WINDOWS XP ,WIRELESS , BLUE TOOTH .

TSHS : 380,000 , 1 YEAR WARRANTY

CALL : 0786 806028
Free Delivery in Dar es salaam

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.

Share this :

Previous
Next Post »
0 Comments