Hawa wabunge wa aina hii hawana lolote, naomba na nataka wananchi wenzangu mniunge mkono ili katika katiba itamke kwamba sifa mama ya mtu kuwa mbunge awe mkazi wa kudumu sio wa kuja na kutoka katika jimbo husika.
Faida mojawapo ya kuishi pamoja na wananchi wako muda wote wa kipindi cha miaka mitano ni kwamba kama tatizo la maji lipo na wewe litakukumba, 0barabara hakuna na wewe litakukumba, umeme pia litakukumba na matatizo mengine yote yatakugusa.
Hii tabia ya watu kujifanya wana uchungu na wananchi huku wakiwa na mahesabu yao na kutaka kupata fedha kupitia ubunge kuna haja ya kuyakomesha.
Ama hilo likishindikana basi iamuliwe kwamba kazi ya ubunge haina mshahara wala posho nono tuone kama mtu apataikana wa kugombea huku akiwa anaishi Dar es Salaam halafu wananchi anaowawakilisha wapo kilomita zaidi 1200 kutoka alipo.
Inanikera sana kuona Wabunge wanawatumia wananchi kama mitaji ya kujitajirisha wao na familia zao, asikudanganye mtu hakuna mbunge anayeweza kufanya kazi ya ajili kusaidia jamii kama wanavyokuwa wanaahidi katika kampeni zao.
Unataka ubunge uwe mkazi wa eneo husika, umeshindwa kutekeleza ahadi zako unapigwa chini hata kama umeongoza mwaka mmoja, umesema uongo ikibainika ulitoa ahadi hewa pigwa chini kabla ya muda wako kumalizika hilo litakuwa fundisho
Ahsante sana ndugu zangu wanabidii kampeni hii idumu
--
Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
0 Comments